Monday, December 9, 2013


SH 2 TRILIONI ZINATOROSHWA KILA MWAKA KUKWEPA KODI

Bunge limeelezwa zaidi ya Dola za Marekani 1.25 bilioni sawa na sh 2 trilionihutoroshwa na kupelekwa nje ya nchi kila mwaka kwa lengo la kukwepa kodi.

Taarifa hiyo imetolewa wakati wingu zito lilikuwa limegubika uwasilishaji wa ripoti ya kikosi cha serikali kilichochunguza sakata la sh 315 bilioni zilizofichwa na watanzania katika mabenki nchini uswisi.
Takwimu hizo zilitolewa juzi na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC), Zitto Kabwe.
Zitto alisema taarifa mbalimbali zinaonesha kuwa Tanzania inapoteza kila mwaka mapato hayo ambayo ni sawa na asilimia tano ya Pato la Taifa kupitia uhamishaji huo haramu.

“Uhamishaji huu haramu wa fedha kupelekwa nje ya nchi hufanywa kwa lengo la kukwepa kulipa kodi au wahusika kuepuka kukamatwa na fedha walizopata kwa kupokea rushwa” alisema Zitto.
Kamati hiyo imependekeza Bunga kupendekeza Bunge kutunga sheria itakayodhibiti uhamishaji haramu au ufichaji wa fedha nje ya lengo la kuogopa kukamatwa na rushwa, kufanya ufisadi na kukwepa kodi.
Zitto alisema hayo ni moja ya maazimio yaliyofikwa katika mkutano wa 10 wa Jumuiya ya kamati za Hesabu za Serikali za Mabunge (Sadcopac) ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (sadc)

Alisema katika mkutano uliofanyika septemba 2 hadi 7 mwaka huu jijini Arusha, wajumbe waliazimia kuhamasisha mabunge ya nvhi zao kutunga sheria kudhibiti uhamishaji huo wa fedha.

0 Responses to “ ”

Post a Comment

More to Read