Friday, February 28, 2014

SERIKALI YA NUNUA BUNDUKI BUNDUKI 500 ZA AK47 KUKABILI UJANGILI


WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII  RAZARO NYALANDU

AK 47


Dar es salaam. Siku moja baada ya Tanzania kutajwa na shirika la polisi la kimataifa (Interpol)kuwa kinara wa biashara ya meno ya tembo Africa Mashariki, Serikali imelipia kodi na kukabidhiwa bunduki 500 aina ya AK47 ili kukabiliana na ujangili katika hifadhi na mapori ya akiba nchini

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu alisema jana kuwa silaha hizo zilikuwa chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), tangu November 2012 kutokana na kutolipiwa kodi zitasambazwa Ngorongoro, selous, pamoja na hifashi za Taifa za Tanapa.

Kati ya shilaha hizo,  250 zitapelekwa kwa idara ya wanyamapori, 200 Tanapa na 50 Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro.

“Silaha hizi jumla y ash 427 milioni kuzinunua lakini zilikwama TRA kwa sababu ya kutolipiwa kodi na ushuru mbali8mbali, hivyo wizara yangu leo inatoa sh 212 milion kwa ajili ya malipo hayo” alisema Waziri Nyarandu.

Alisema silaha hizo zimekombolewa ikiwa sehemu ya kutekeleza maazimio ya Bunge na ahadi ya serikali kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maliasili ,Ardhi na Mazingira.

Akizungumzia sababu za kuchelewa TRA, Nyarandu amesema kulikuwa na ubishi wa ama zilipaswa kulipiwa kodi au la, lakini mamlaka hiyo ilifafanua kuwa h ayo ndiyo matakwa ya sheria, hivyo akaamua kutoa fedha hizo.

Silaha hizo zimepatikana ikiwa ni takribani wiki mbili tangu Raisi Jakaya Kikwete abanwe  na vyombo vya habari vya kimataifa akitakiwa kueleza mikakati iliyopo kupambana na ujangili ambao umeharibu sura ya Tanzania nje ya nchi.

Itakumbukwa kuwa miezi miwili iliyopita , Rais Jakaya Kikwete alilazimika kupangua Baraza la Mawaziri na kuwatimua mawaziri wane kutokana na vitendo vya kinyama vilivyobainishwa na kamati ya Bunge ya Maliasili na Mazingira wakati wa operesheni Tokomeza Ujangili.

Majangili papa 40
Akijibu maswali ya waandishi wa habari, Waziri Nyarandu alisema majina ya majangili papa 40 ambayo Rais Kikwete alisema anayo, ‘yatabandikwa’ hivi karibuni .


Amesema, Serikali inawafahamu majangili hao kwa udani, wanapokunywa chai,wanapotembelea na shughuli zao za kila siku.

Amesema majina yao si siri kwani tayari wameshafunguliwa mashtaka na wapo chini ya mfumo wa mahakama na wamekamatwa na vidhibiti.

Hivi karibuni, Rais Kikwete alihojiwa na shirika la utangazaji la Uingereza( BBC),  alisema serikali ina majina 40 ya majangili papa na mkuu wao yuko Arusha.

Selous Yaimarishwa
Katika  hatua nyingine, waziri Nyarandu alitangaza kuzipandisha hadhi kand nane zalizopo katika pori la Akiba la Selous, ili ziweze kujitegemea kiutendani kwa kuweka mkuu wa kila kanda.

Alisema pori hilo lina ukubwa unaokaribia hifadhi zote za Taifa chini ya Tanapa ,  jambo linalolifanya kuwa kubwa kimenejiment na kuuendeshaji.

Pori la selous lina kilomita za maraba 55,000 wkati mapori yote nchini kwa ukubwa wake ni kilomita za mraba 57,000 .

Katika kuweka mazingira ya uangalizi wa kina ya kupambana na ujangili, aliiagiza idara ya Wanyamapori kukamilisha mchakato wa kufungua akaunti maalumu za benki kwa kila kanda ili kuwawezesha wakuu wa kand kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

0 Responses to “SERIKALI YA NUNUA BUNDUKI BUNDUKI 500 ZA AK47 KUKABILI UJANGILI”

Post a Comment

More to Read