Friday, February 28, 2014

BANDARI YA DAR ES SALAAM KUANZA KUTOA HUDUMA MASAA 24


BANDARI YA DAR ES SALAAM


Dar es salaam. Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ikishirikiana na wadau wake kuanzia kesho wanatarajia kuanza kutoa huduma kwa saa 24, siku saba katika wiki, mwaka mzima bila kupumzika.

Ofisa Uhusiano wa TPA, Janeth Zurngi alisema uamuzi huo ambao unakusudia kuongeza ufanisi wa bandari hiyo, umefikiwa baada ya wadau mbalimbali kutia saini mikataba ya utekelezaji kazi hiyo.

Zurangi Amesema ingawa kulikuwapo mabishano kuhusu vipengele kadhaa ndani ya mkataba huo, wadau wote walikubali kuanza kutoa huduma kila siku kwa saa 24 kuanzia Machi Mosi.

“Mwezi  ujao utaratibu huo utaanza na tunatarajia utakuwa na mafanikio makubwa. Hivi sasa mteja anaweza kuchelwa kuchukua mzigo kwa sababu baadhi ya wadau hawajasaini vibali husika”, alisema.

Oktoba 14 mwaka jana , Waziri wa Uchukuzi, DK Harrison Mwakyembe aliwataka wadau wengine wanaofanya kazi TPA kuanzisha utaratibu wa kufanya kazi kila siku, kwa  kile alichoeleza kutofanya hivyo kunakwamisha kasi ya uondoaaji mizigo bandarini.

DK Mwakyembe alinukuliwa akisema: “Bandari wanafanya kazi saa 24 kwa siku saba za wiki bila kupumzika, lakiniwenzetu wa TRA wao sikukuu na siku za mwisho wa juma wanalala hali hii itaturudisha nyuma kimapato

” Baadhi ya wadu walisaini mkataba huo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Chama cha Wakala wa Forodha na Uondoshaji Shehena Tanzania (Taffa)

0 Responses to “BANDARI YA DAR ES SALAAM KUANZA KUTOA HUDUMA MASAA 24 ”

Post a Comment

More to Read