Wednesday, March 19, 2014
MSAKO WA NDEGE WAANZA ARDHINI CHINA.
Do you like this story?
Serikali ya China imeanza juhudi za
kuitafuta katika ardhi yake ndege ya Malaysia iliyotoweka mwishoni mwa wiki
jana.
Hii ni sehemu ya juhudi za kimataifa
zinazoendelea kuitafuta ndege hiyo.
Wataalamu wanaoendesha shughuli hiyo
wanalenga zaidi maeneo mawili ya nchi hiyo, Kaskazini na Kusini.
China imesema kuwa hakuna abiria
yeyote wa nchi hiyo aliyekuwa katika ndege hiyo amehusishwa na ugaidi.
Ndege hiyo ilitoweka tarehe 8 mwezi
Machi ikiwa imewabeba watu 239.
Nchi 26 zinahusika na msako huo.
Malaysia inasema kuwa ndege hiyo
ilibadili mkondo na huenda ilipaa kuelekea Kusini au Kaskazini.
Wapelelezi wanachunguza uwezekano wa
ikiwa abiria au rubani na rubani mwenza walihusika na tukio la kutoweka kwa
ndege hiyo.
Raia 153 wa China walikuwa katika
ndege hiyo ambayo ilikuwa inatoka Malaysia kuelekea mjini Beijing, China.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MSAKO WA NDEGE WAANZA ARDHINI CHINA.”
Post a Comment