Friday, March 7, 2014

MVUA ZAWAWEKA ROHO JUU WAKAZI DAR.


Dar es salaam


Mvua zinazoendelea kunyesha jijini dar es salaam, zimezua taharuki kwa wakazi wake hasa baada ya kusababisha athari katika baadhi ya maeneo muhimu.

Moja ya maeneo hayo ni hospitali ya palestina iliyopo sinza ambayo ilijaa maji na kusababisha usumbufu mkubwa.

Mganga mkuu wa hospitali hiyo . DK benedict luoga amesema mvua hizo zilizonyesha juzi zilisababisha maji kuingia katika moja  ya majengo yake.

Amesema kutokana na hali hiyo, shughuli katika hospitali zilisimama kwa muda hadi kazi za kutengeneza njia mbadala ilipokamilika.

“Tumeshapeleka malalamiko yetu kwenye mamlaka husika lakini hakuna kinachofanyika. Tulichoamua kufanya sasa ni kujenga tuta la kingo ili kuziua maji yaiingie ndani hasa katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendela kunyesha” alisema .

Katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo baadahi ya barabara na mifereji ya maji machafu ilionekana ikiwa imejaa maji na kusababisha foleni kutoka na madereva kuendesha magari kwa tahadhari.

Baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na mvua hizo ni vingunguti, sinza, kipawa, jangwani,kariakoo na kigogo.

0 Responses to “MVUA ZAWAWEKA ROHO JUU WAKAZI DAR.”

Post a Comment

More to Read