Friday, March 7, 2014

MUHONGO AONGEZA UTATA MABILIONI YA IPTL.


Waziri wa nishati na madini profesa Sospeter Muhongo


Wakati utata wa kuchotwa kwa fesha katika akaunti ya Escro iliyofunguiwa katika benki kuu ya Tanzania (BoT) kutokana na mgogoro baina ya IPTL na Tanesco ukiendelea kuzua maswali, waziri wa nishati na madini profesa Sospeter muhongo amesema fedha hizo hakzikuwa za serikali.

“Hizo fedha hazikuwa za serikali, Tanesco ilitakiwa kulipa Capacity charge(gharama za uwekezaji) kwa IPTL kama inavyolipa karibu sh 27 billioni kwa kampuni nyingine zinazozalisha umeme” alisema profesa muhongo.

Itakumbukwa kuwa kutokana  na mgogoro wa IPTL na Tanesco akaunti hiyo ilifunguliwa ili fedha ambazo Tanesco ilipaswa kulipa IPTL kwa ajili ya capacity charge ziwekwe kwenye akaunti hiyo hadi mgogoro huo utakapomalizika.

Kwa kuwa malalamiko yalikuwa kwamba, fedha Ambazo Tanesco ilikuwa ikiilipa IPTL zilikuwa nyingi kuliko ilivyostahili, ilitarajiwa kwamba baada ya kesi iliyofuguliwa marekani kuamuriwa, ingepatikana njia kukokotoa gharama halisi na sehemu ya fedha hizo kurudi Tanesco.

Sehemu ya taarifa kwa umma iliyotolewa na ofisi ya uhusiano Tanesco Makao makuu jumanne iliyopiga kufafanua taarifa zilizokuwa zimeandikwa juu ya hukumu hiyo inasema mahakama hiyo (ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya uwekezaji) haikutangaza aliyeshinda wala kushindwa

Ilichofanya ni kutoa muda wa miezi mitatu pande zeote mbili,(standard chartered bank) Hong kong(SCB-HK)  na Tanesco kwenda kukubaliana nje ya mahakama kwa sasa kuna mazungumzo yanayoendelea kuhusu taratibu za kukokotoa  gharama halisi.

Profesa muhongo alipoulizwa iwapo serikali inaitambua SCB- HK na hukumu iliyotolwa na mahakama hiyo ya kimataifa alisema kwa kifupi “kwani sisi tunaendeshwa na sheria za marekani?he gai wabia wengine wanatambua SCB-HK?

Pia hakutaka moja kwa moja kukiri kuwa serikali ndiyo iliyotoa fedha hizo na kuzitoa kwa pan African power solution wala kukanusha taarifa hizo, badala yake alisema swali hilo waulizwe wahusika katika suala hilo.

0 Responses to “MUHONGO AONGEZA UTATA MABILIONI YA IPTL.”

Post a Comment

More to Read