Friday, March 7, 2014

WARAKA MZITO WA RAC KWA LORD EYEZ.


Ray c


Staa wa bongo fleva , Rehema chalamila ‘Ray c’almaarufu kiuno bila mfupa amemwandikia waraka  mzito aliyewahi kuwa mwandani wake,Rapa waziri makato ‘lord EYez ‘ akimtaka kubadili ‘laifu staili yake.

Ray c  alimwandikia wakala huo lord Eyez  wa Nako2 Nako solders juzi ikiwa ni saa chache tangu alipo simamishwa kazi katika kampuni ya weusi  baada ya kutuhumiwa  kwa  wizi wa kompyuta  mpakato (laptop)  jijini Arusha ivi kalibuni.

Huku akitanguliza picha ya ‘Mnato ‘ huku  akisindikizwa  na polisi , Ray c aliandika waraka  huo kwenye ukurasa wake wa instagram.
‘’Badilika babaa… nakuombea sana ujitambue  na ubadili mwenendo  wa maisha  yako…wewe bado kijana mdogo sana  na unakipaji cha kipekee.

‘’kila mtu ana changamoto yake  ya kimaisha …angalia wapi ulipokosea, litambue  tatizo lako alafu kubali kwamba  unatatizo   halafu rekebisha  hilo tatizo …anza maisha mapya .

‘’Badili …majanga yote  yanayo kukuta  ni ishara tosha  kutoka kwa mwenyezi mungu  kwamba unakoelekea siko.’
‘’kama una akili timamu  basi utagundua hilo utajilekebisha babaa.

0 Responses to “WARAKA MZITO WA RAC KWA LORD EYEZ.”

Post a Comment

More to Read