Wednesday, October 28, 2015
DIAMOND: KAWEKA HISTORIA ULAYA
Do you like this story?
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’. |
Andrew Carlos na Musa Mateja
OKTOBA 25, mwaka huu ilikuwa ni
moja kati ya siku za kihistoria nchini kwa Watanzania wote kujumuika na kupiga
kura za kuwachagua wabunge, madiwani na rais.
Siku hiyohiyo pia katika Jiji la Milan,
Italia kulikuwa na tukio la kihistoria kwa staa wa muziki wa Bongo Fleva,
Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye alikuwa akiiwakilisha Tanzania na Afrika kwa
ujumla katika Tuzo za MTV Europe Music (EMA) na kufanikiwa kuibuka na ushindi
kupitia kipengele cha Best Worldwide Act: Africa/India ambacho alikuwa
akichuana na mwanamuziki maarufu wa India, Priyanka Chopra aliyewahi kuwa pia
Miss World mwaka 2000.
Uso kwa uso na mastaa ulaya
Kati ya matukio ambayo Diamond anasema hawezi
kuyasahau ni pamoja na kupata shavu la kukutana na mastaa kibao wa ulaya ambao
walipafomu na wengine kuchukuwa tuzo.
“Nimekutana na mastaa wengi ambao sikuwahi
kukutana nao kabisa zaidi ya kuwaona tu kwenye mitandao na TV. Mastaa hao ni
pamoja na Jason Deluro ambaye pia alipafomu Wimbo wa Want to Want, Pharrel Williams
naye alipafomu Wimbo wa Freedom.“Nilipata bahati pia ya kuwashuhudia mastaa
wengine kama vile Justin Bieber, Ed Sheeran na wengine kibao,” alisema Diamond.
Bieber anyakua 5 kwa mpigo
Staa wa Pop, Justin Bieber aliweka historia
kwake katika tuzo hizo baada ya kuibuka na tuzo tano kwa mpigo.
Staa huyo aliyepanda jukwaani na kupiga ngoma yake mpya ya What Do You Mean alifanikiwa kuibuka na tuzo katika vipengele vya Best Male, Best Look, Worldwide Act: North America, Biggest Fans na Best Collaboration.
Staa huyo aliyepanda jukwaani na kupiga ngoma yake mpya ya What Do You Mean alifanikiwa kuibuka na tuzo katika vipengele vya Best Male, Best Look, Worldwide Act: North America, Biggest Fans na Best Collaboration.
Mastaa wengine waliochukua tuzo hizo ni Nicki Minaj, One Direction, Macklemore, Taylor Swift, Ed Sheeran, Rihanna na wengine kibao.
Wazungu wapagawa na Diamond
Katika hali ya kushangaza mapema kabla ya
kuanza kwa sherehe hizo za utoaji tuzo, Diamond aliyekuwa amevalia suti nyeupe
alitinga ‘red carpet’ na kushangaa kuvamiwa na wazungu waliookuwa wamepanga
foleni kuwasubiri mastaa huku kila mmoja akiwa na simu yake mkononi akitaka
kupiga picha naye (selfie).
Washindi waliopita
Katika kipengele alichoshinda Diamond,
alitanguliwa na Abdelfattah Grini (Morocco) aliyechukuwa mwaka 2011, Ahmed
Soultan (Morocco) mwaka 2012 na 2013 na wa mwisho alikuwa Mohamed Assaf
(Palestina).
Diamond anasemaje?
Kutokana na ushindi huo uliokuja Tanzania na
Afrika kwa ujumla, Diamond alifunguka mengi ya kushukuru kwa wale wote
waliompigia kura na kuahidi kufanya makubwa zaidi ya hayo katika kazi zake za
muziki.
“Nimeshangazwa sana kwa namna ambayo
nimepokelewa kwa kishindo nchini Italia. Wazungu wamenionesha thamani ya juu
kwa mapokezi makubwa na kunishangilia na kunipongeza kwa tuzo niliyoipata.
Nasema asanteni sana Watanzania wenzangu kwa sapoti mlionionesha mwanzo mwisho
hadi kwa kunipigia kura na kufanikiwa kuibuka mshindi kutoka Afrika,” alisema
Diamond.
Diamond alifanikiwa kupita tano bora Afrika
katika Tuzo za Ema baada ya kupigiwa kura za kutosha na mashabiki wake kupitia
mtandao wa Twitter. Wasanii wa Afrika aliokuwa akichuana nao kabla ya kutua
Italia ni Yemi Alade (Nigeria), Davido (Nigeria), AKA (Afrika Kusini) pamoja na
Wizkid (Nigeria).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ DIAMOND: KAWEKA HISTORIA ULAYA”
Post a Comment