Wednesday, October 28, 2015
TUME YA UCHAGUZI IMEFUTA MATOKEO YOTE YA UCHAGUZI MKUU ZANZIBAR
Do you like this story?
Tume ya Uchaguzi Zanzibar imeufuta
uchaguzi mkuu wa Zanzibar kutokana na kuwa
na dosari nyingi ikiwemo uchaguzi kutokuwa
huru na wahaki
Mwenyekiti wa ZEC ametoa
tangazo hilo kupitia shirika la utangazaji la ZBC
mchana huu kuwa amechukua maamuzi hayo
baada ya kujiridhisha kuwa uchaguzi
uligubikwa na dosari nyingi.
"Mimi nikiwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, nimeridhika kuwa Uchaguzi huu umegubikwa na makosa makubwa....
"Kwa mamlaka niliyonayo natangaza rasmi kuufuta
uchaguzi huu kwa kuwa haukuwa huru na wa haki, mtajuulishwa tarehe
itakayofanyika uchaguzi mwengine hapo baadae, Ahsanteni kwa kunisikiliza"!
- Jecha S. Jecha, Mwenyekiti wa
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ TUME YA UCHAGUZI IMEFUTA MATOKEO YOTE YA UCHAGUZI MKUU ZANZIBAR”
Post a Comment