Wednesday, October 28, 2015
LOWASSA APINGA MATOKEO YA UCHAGUZI
Do you like this story?
Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha CHADEMA Edward LOwassa
amesema kuwa hatokubali matokeo ya uchaguzi wa urais yanayoendelea kutolewa na
tume ya uchaguzi nchini Tanzania NEC.
Amesema kuwa ana ushahidi wa kutosha kwamba kuna udanganyifu
uliofanyika.
Amesema kuwa kura za chama hicho zimepunguzwa katika vituo vingi vya
kupigia kura.
Wanadai kwamba kura zilizohesabiwa katika maeneo tofauti haziambatani
na matokeo yaliotolewa.
Lowassa ameongezea kwamba maeneo yote ambayo walipata ushindi
yamecheleweshwa huku kukamatwa kwa maajenti wa chama hicho akidai kuwa ni
ishara za kutaka kuiba kura.
Chanzo BBC Swahili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ LOWASSA APINGA MATOKEO YA UCHAGUZI ”
Post a Comment