Saturday, April 12, 2014
AZAM FC YATUA JIJINI MBEYA TAYARI YAANZA MAZOEZI KWAAJILI YA KUJIANDAA NA MECHI ZIDI YAKE NA MBEYA CITY.
Do you like this story?
KIKOSI cha vinara wa ligi kuu soka
Tanzania bara, Azam FC, kinaondoka asubuhi ya leo Dar es Salaam kwa ndege
kwenda jijini Mbeya kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu sokaTanzania Bara dhidi ya
wenyeji Mbeya City kwenye Uwanja wa
Sokoine mjini humo.
Azam fc wanakwenda Mbeya kuhitaji pointi tatu ambazo zitawapa ubingwa rasmi na kuwavua mabingwa watetezi, Dar Young Africans.
Kocha Mcameroon wa Azam FC, Joseph
Marius Omog alikuwa mwenye furaha baada ya ushindi wa 3-0 juzi Uwanja wa
Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani dhidi ya wenyeji Ruvu Shooting, lakini akasema
shughuli haijaisha.
“Ni furaha. Ni ushindi mzuri, tumevuka
kikwazo kimoja, vijana waliuanza mchezo vizuri wakizingatia nilichowaambia.
Karibu kila mmoja alitekeleza majukumu yake vizuri. Wapinzani walikuwa wagumu,
lakini tumechukua pointi tatu,”alisema.
Omog alisema anajivunia wachezaji wake
na hana cha kuwaambia zaidi ya asante pamoja kama timu na akawataka kuendeleza
mshikamano huo daima.
Hata hivyo, Omog amewaambia wachezaji
wake kwamba wanahitaji kushinda pia mechi mbili za mwisho ili wamalize ligi
vizuri.
Ushindi huo umeifanya Azam FC ifikishe pointi 56 baada ya kucheza mechi 24 na kujivuta karibu kabisa na chumba kinachohifadhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu, ikiwaacha kwa pointi nne mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 52 za mechi 24 pia.
Timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake, baada ya mechi ya kesho itacheza mechi ya mwisho dhidi ya JKT Ruvu Aprili 19, Uwanja wake wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AZAM FC YATUA JIJINI MBEYA TAYARI YAANZA MAZOEZI KWAAJILI YA KUJIANDAA NA MECHI ZIDI YAKE NA MBEYA CITY.”
Post a Comment