Friday, February 12, 2016

"KINNAH PHIRI" AMESEMA MBEYA CITY ITAFIKA NAFASI YA NNE LIGI KUU TANZANIA BARA.


Kocha Mkuu wa timu ya Mbeya City Kinnah Phiri(Picha na David Nyembe wa Fahari News)
                             
Kocha Mkuu wa timu ya mbeya city Mmalawi Kinnah Phiri ameweka bayana kuwa hakuna kinacho shindikana kwa kikosi cha kumaliza kwenye nafasi nne za juu kwenye msimamo  wa ligi kuu ya soka Tanzania bara inayotaraji kuendelea kwenye viwanja mbalimbali wikiendi hii.

Akiongea na waandishi wa habari kwenye hotel ya Maunt Living Stone jijini mbeya leo hii Phiri amesema kuwa hata alipokuwa nchini kwao Malawi iliwahi kutokea timu mbili zilizokuwa zinaongoza kwa kipindi kirefu katika ligi zilimaliza kwenye nafasi mbili za mwisho ligi hiyo ilipofika tamati.

Aidha kocha huyo aliyesaini mkataba wa miaka mitatu kuchukua mikoba ya meja mstaaf Abdul Mingange hivi karibuni amewataka mashabiki na wapenzi wa klabu ya Mbeya City kutambua kuwa sasa hivi wamepata kocha ambaye anataraji kurejesha makali ya wagonga nyundo hao wa Mbeya

Kwa upande mwingine mwalimu huyo amefahamisha kuwa ataanza kuiingiza ufundi wake taratibu ili kuepusha kuichanganya timu na mwishoni mwa msimu ndipo atakapo weza kuuukita mfumo wake na kuweka bayana kuwa aina gani ya wachezaji atakaokwenda sambamba na mbio zake za kurejesha makali ya Mbeya City



0 Responses to “"KINNAH PHIRI" AMESEMA MBEYA CITY ITAFIKA NAFASI YA NNE LIGI KUU TANZANIA BARA. ”

Post a Comment

More to Read