Saturday, February 13, 2016

KOCHA WA TIMU YA MBEYA CITY KINNAH PHIRI AMEANZA VYEMA KUIONGOZA TIMU HIYO KWA KUPATA USHINDI WA MABAO 5-1 DHIDI YA TOTO AFRICAN YA MWANZA.


Kikosi cha Mbeya City(Picha na David Nyembe wa Fahari News)










Kocha wa timu ya Mbeya City Kinnah Phiri ameanza vyema kuiongoza timu hiyo kwa kupata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Toto Africans kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya

Tangu timu hiyo ipande ligi kuu ya soka haijawahi kupata ushindi mkubwa kama huo ambapo kiungo Raphael Alfa alikuwa wakwanza kuiandikia bao kwanjia ya mkwaju wa penati mnamo dakika ya tano ya mchezo kufuatia walinzi Toto kumfanyia madhambi kiungo mshambuliaji wa Mbeya City Ditrim Nchimbi

Ramadhani chombo aliipatia Mbeya City bao la pili kwenye dakika ya 35 baada ya kuunganisha kwa kichwa Krosi iliyopigwa na Haruna Moshi baada ya kupokea pasi iliyotoka kwa mfungaji Ramadhani Chomo

Mbeya city wakionekana wenye uchu wa mabao waliandika bao la tatu kupitia kwa Haruna Moshi aliyefanikiwa kuihadaa ngome ya wana kishamapanda katika dakika ya 41 kisha akaongeza bao la nne mnamo dakika ya 43
Mpka timu hizo zinakwenda mapumziko Mbeya City 4 Toto Africans 0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo kila upande ukihitaji matokeo na ikamlazimu Kocha Kinnah Phiri wa Mbeya City kumuingiza kiungo mshambuliaji mwenye kasi Meshack Samweli aliyeingia kuchukua nafasi ya Ramadhani Chombo ambapo mpira wakwanza aliokutana nao akaiandikia Mbeya City bao la tano kunako dakika ya 79 kufuatia krosi Murwa iliyopigwa na Ditrim Nchimbi , bao lakufutia machozi la Toto Africans ya Mwanza limefungwa na Japhet Mkala dakika ya 78.

Mpaka mwamuzi wa mchezo huo anapuliza kipyenga kuashiria kumalizika kwa dakika 90 za mchezo Mbeya City 5 Toto Africans 1

0 Responses to “ KOCHA WA TIMU YA MBEYA CITY KINNAH PHIRI AMEANZA VYEMA KUIONGOZA TIMU HIYO KWA KUPATA USHINDI WA MABAO 5-1 DHIDI YA TOTO AFRICAN YA MWANZA. ”

Post a Comment

More to Read