Tuesday, February 16, 2016
HUDUMA MPYA YA KITABIBU YAANZA KUTOLEWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA MBEYA.
Do you like this story?
Upasuaji Ukiendelea (Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Mwonekano wa Mashine ya Mnara wa Upasuaji wa Vitundu( Laparoscopic)(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Prof. Dr Med Henning Kushoto akiwa na Frorian Beatz Mara Baada ya kumaliza Upasuaji Mgojwa wa Kwanza(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Huduma
mpya ya kitabibu imeanza kutolewa katika hospitali ya rufaa ya kanda ya Mbeya
itakayomuwezesha mgonjwa kufanyiwa upasuaji kwa njia ya vitundu (Laparoscopic
surgery) na hivyo kumuwezesha mgonjwa kupona mapema na kuwahudumia wagonjwa
wengi kwa muda mfupi.
Huduma hiyo ambayo inatumia mashine
inayofahamika kwa jina la Mnara wa Upasuaji wa Vitundu au Laparascopic Tower
inalenga kutumia muda mfupi wa upasuaji, na kumuwezesha kufanya mgonjwa kupata
naafuu mapema.
Akizungumza
na mwandishi wetu daktari bingwa wa Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya kanda
ya Mbeya, Dkt. Lazaro Mboma amesema kuwa mashine hiyo itamuwezesha mgonjwa
kurudi katika shughuli zake za kawaida muda mfupi baada ya upasuaji kutokana na
kutokuwa na kidonda kikubwa badala yake mgonjwa atakuwa akiuguza vidonda vidogo
vya matundu yaliyotumika wakati wa upasuaji tu.
Pamoja na hayo amesema kuwa kwa siku ya kwanza
(leo) wagonjwa wawili waliokuwa na matatizo ya mawe katika mfuko wa nyongo
wamefanyiwa upasuaji wa mafanikio ambapo kazi hiyo imekwenda sambamba na kuwapa
mafunzo madaktari wengine wa hospitali hiyo juu ya matumizi ya mashine hiyo.
Aidha
Dkt. Lazaro Mboma kuwa mashine ya Mnara wa Upasuaji wa Vitundu inawahusu
wagonjwa wote, wale wanaotumia bima za afya na wasionazo lakini kutokana na gharama
za uendesheji inawalazimu madaktari kuwahudumia kwanza wagonjwa wanaohudumiwa
kwa bima ya afya kwani hivyo amewashauri wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya
afya kwani kwa mgonjwa wa kawaida ni ngumu kumudu gharama za matibabu.
Madaktari waliofika jijini Mbeya kwaajili ya kutoa mafunzo kwa madaktari wa
hospitali hiyo ni daktari Prof. Hening na mtaalamu wa mashine hiyo Frolian Bets
ambao wataendelea kuwepo jijini Mbeya kwa siku tatu ili kuwawezesha madaktari
wa hospitali ya Rufaa Mbeya kupata ujuzi wa kutumia mashine hiyo.
Naye
mkuu wa idara ya upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya Mbeya Dkt.
Mujuni Mutagwaba ametoa wito kwa wakazi wa Mbeya na mikoa ya nyanda za juu
kusini kujitokeza kutibiwa katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya Mbeya ili
kuokoa gharama na kupata tiba stahiki.
Mashine
ya kitabibu ya Mnara wa Upasuaji wa Vitundu (Laparoscopic Tower) ni ya kwanza
mkoani Mbeya na ni vituo vichache Tanzania vilivyo na mashina ya upasuaji ya
aina hii hivyo kupelekea wagonjwa wengine kusafiri kwenda nchi nyingine
kwaajili ya kupata tiba kwa njia hii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HUDUMA MPYA YA KITABIBU YAANZA KUTOLEWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA MBEYA.”
Post a Comment