Friday, February 19, 2016

DABI YA SIMBA NA YANGA KUPIGWA KESHO.




Ligi kuu ya Tanzania bara itaendelea tena hapo kesho kwa jumla ya michezo sita kuchezwa.

Macho na masikio ya wapenda soka yatakua yakisubiri kwa hamu Dabi ya kariakoo kati ya Wekundu wa msimbazi Simba Sport Klabu, dhidi ya timu ya wananchi Dar Young Afrikans Yanga, mchezo utakaopigwa kwenye dimba la taifa Jijini Dar Es Salaam.

Michezo mingine itayaopigwa hapo kesho Mgambo Jkt wataonyeshana ubavu na Tanzania Prisons, Stand United wao watawalika Jkt Ruvu.

Mbeya City wao watakua nyumbani Sokoine kukupiga na Wanalambalamba Azam FC , huku wanalizombe Majimaji wakikipiga na wakata miwa wa Mtibwa Sugar .Toto Africans ya Mwanza, wao watawalika jirani zao kutoka mkoani Kagera, Kagera Sugar.

0 Responses to “DABI YA SIMBA NA YANGA KUPIGWA KESHO.”

Post a Comment

More to Read