Friday, February 19, 2016
WAKATI BEI ZA HUDUMA YA UPASUAJI WA VITUNDU IKIPANGWA RUFAA MBEYA, WENYE BIMA ZA AFYA WAENDELEA KUNUFAIKA
Do you like this story?
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Thomas Isdory akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Prof Daktari Bingwa kutoka German Herning pamoja na Madaktari kutoka Hospitali ya Rufaa Mbeya wakiwa katika Upasuaji. (Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Na Nebart Msokwa,
Mbeya
BAADA ya muda mrefu
wananchi kufuata huduma za upasuaji kwa njia ya teknolojia mpya ya Vitundu
nchini India, Hospitali ya Kanda ya Rufaa Mbeya imeanza kutoa huduma na hiyo
kupunguza gharama kubwa za kusafirisha wagonjwa kwenda nje ya nchi.
Huduma hiyo ilizinduliwa juzi ambapo ilitanguliwa na
semina pamoja na mafunzo kwa wataalamu juu ya namna ya kuvitumia vifaa ambavyo
ni vipya kwao, na baadaye kufanya kwa vitendo kwa kufanya upasuaji wa wagonjwa
Saba.
Madaktari Bingwa wa
upasuaji katika Hospitali hiyo ya kanda ya Mbeya, waliungana na wataalamu
kutoka Ujerumani ambao ndio walioleta neema hiyo ambayo inajulikana kama
upasuaji kwa njia ya vitundu inayojulikana kwa jina la kitaalamu ‘Raparascopic
Tower’
Kaimu Mkurugenzi wa
Hospitali hiyo Thomas Isdory, alisema kuwa huduma hiyo ya Upasuaji kwa kutumia
teknolojia ya Vitundu, imeanzia kwa wananchi wote ambao ni wanachama wa Mfuko
wa taifa wa Bima ya Afya.
Amesema kuwa wameanza
na wanachama wa mfuko huo kutokana na kwamba mfuko huo tayari ulishatoa gharama
za matibabu kwa kutumia teknolojia hiyo na kwama utaratibu kwa wananchi wengine
utaanza baadaye.
Isdory amesema kuwa
changamoto kubwa inayoikabili Hospitali hiyo ni uhaba wa madaktari bingwa,
ambapo amesema kuwa hospitali ina madaktari bingwa wa upasuaji wanne tu ambao
hawatoshi kulingana na mahitaji.
Alifafanua kuwa kati
ya madaktari bingwa hao wawili wapo katika kitengo cha upasuaji wa akina mama
Meta huku wengine wawili wakiwa katika Hospitali kuu wakifanya upasuaji wa
magonjwa ya kawaida.
“ Kwa kuanzia
tumeanza na wagonjwa ambao ni wateja wa mfuko wa bima ya Afya kutokana na
kwamba wenzetu wa Bima tayari walishatangaza bei za matibabu kwa kutumia
teknolojia hii mpya, lakini taratibu zinaendelea kupanga bei kwa ajili ya watu
wengine ili wote waweze kuipata,” alisema Isdory.
Guydon Makulila
ambaye ni Mtaalamu wa Dawa za Usingizi amesema kuwa teknolojia hiyo ni nzuri
kuliko ile ya kuchana kutokana na kwamba yenyewe mgonjwa hapati maumivu makali
kutokana na kwamba vinatobolewa vitundu vidogo.
Amesema kuwa pia
haina hatua nyingi kutokana na kwamba mgonjwa hukaa kwenye dawa kwa muda mfupi
kabla ya kufanyiwa upasuaji huo na kwamba hakuna mgonjwa kurudi tena Hospitali
kwa ajili ya kutoa nyuzi.
Alidai kuwa mgonjwa
hupata nafuu haraka kuliko ile ya kuchana na kwamba mgonjwa hupana fahamu baada
ya muda mfupi na kuweza kujieleza vizuri tofauti na ile ya zamani.
“Operasheni kwa
kutumia teknolojia hii ni nzuri sana maana haina mgonjwa hapati maumivu makali
sana kama ilivyo kwa ile ya kuchana, hakuna mgonjwa kukaa muda mrefu kwenye
dawa, pia mgonjwa hupata nafuu haraka na hakuna kurudi ili kutolewa nyuzi,”
alisema Makulila.
Nao baadhi ya
wagonjwa waliokuwa wamefanyiwa upasuaji kwa kutumia teknolojia hiyo akiwemo
Edda Kayinga na Anna Edward ambao wote walitolewa mawe kwenye mfuko wa nyongo
walisema kuwa huduma hiyo ni nzuri kutokana na kwamba inafanyika haraka
na hata maumivu yanakuwa ya kawaida.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAKATI BEI ZA HUDUMA YA UPASUAJI WA VITUNDU IKIPANGWA RUFAA MBEYA, WENYE BIMA ZA AFYA WAENDELEA KUNUFAIKA”
Post a Comment