Monday, May 26, 2014
KANDORO ATULIZA HASIRA ZA WANANCHI MARA BAADA YA KUFUNGA BARABARA KWA MASAA KADHAA
Do you like this story?
Wananchi wakiwa barabarani huku
wakiwa wamepanga magogo kushinikiza kuonana na mkuu wa mkoa wa mbeya mara baada
ya mwananchi mwenzao kugongwa na kufa papo hapo
|
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizungumza kwa msisitizo na wananchi hao |
Mwili wa Marehemu ukiwa chini
pembezo mwa Barabara
|
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya
Ahmed Msangi baada ya kuzungumza kwa kuwasihi wananchi hao kutotumia sheria mkononi(Picha na fahari news)
|
WANANCHI wa kijiji
cha Nanyala Wilayani Mbozi, leo
wamefunga barabara kuu ya Tanzania- Zambia zaidi ya masaa
matano na kusababisha kukwama kwa wasafiri waendeo nchi za kusini mwa Afrika na
jijini Dar es Salaam.
Wananchi hao ambao
waliamua kutumia maiti ya mtoto wa miaka mitano Alfani Dumu ambaye aligongwa na
gari ndogo ya abiria (HICE) kwa kuilaza barabarani hivyo kusababisha usumbufu
mkubwa kwa watumiaji wa njia hiyo.
Wakizungumza kwenye eneo la tukio, walisema tukio hilo
limetokea majira ya saa tatu za asubuhi mara baada ya marehemu mtoto huyo akiwa
anavuka barabara akitokea shuleni kugongwa na gari hilo.
Akielezea sababu ya
wao kufunga barabara hiyo, Mmoja wa wananchi hao ambaye hakutaka kutaja jina
lake amesema wamechoshwa na ahadi hewa za
serikali kwa kushindwa kuwatekelezea ombi lao la kuiweka barabara hiyo
matuta, alama za barabarani pamoja na askari wa usalama barabarani ambaye
atakuwa na tochi.
Amesema Zaidi ya
miaka mitatu wamekuwa wakipigia kelele suala hilo lakini hakuna utekelezaji wa
aina yoyote uliofanyika .
tumeiomba serikali
kuangalia uwezekano wa eneo hili la barabara
Akizungumzia tukio
hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro, amewataka wakazi hao kuondoa maiti
hiyo kisha kufungua njia ili watumiaji waweze kuitumia kwani suala lao
amelipokea na kwamba atalifanyia kazi.
Aidha Mkuu huyo wa
Mkoa ameliagiza jeshi la polisi mkoani humo kuhakikisha linaweka askari wa
usalama barabara kwa muda wote katika eneo hilo pamoja na kuhakikisha kuwa
askari hao wanakuwa na vifaa vya kupimia mwendo kasi.
Amesema kwa dereva
yoyote atakaye kwenda kinyume na taratibu ameagiza kuchukuliwa kwa hatua
kali kwa lengo la kukomesha vitendo hivyo.
Aidha, Kandoro
amemuagiza Wakala wa barabara nchini(TANROAD) Mkoa wa Mbeya, kulifanyia
matengenezo eneo hilo kwa kuweka matuta pamoja na alama za barabarani mapema
kesho badala ya kuchukua muda mrefu.
Naye Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, aliwahakikishia usalama wakazi hao na
kwamba askari wa tochi watakuwa kwenye eneo hilo huku akiwasisistiza kuacha
tabia ya kujichukulia sheria mkononi mara vitendo vya uhalifu
vinapotokea.
Hata hivyo mara
baada ya mkuu huyo wa mkoa kuzungumza na wananchi haio na kuwasihi kufungua
barabara hiyo mara moja wananchi hao walitii agizo hilo na usafiri kuendelea
kama kawaida majira ya saa3 jioni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KANDORO ATULIZA HASIRA ZA WANANCHI MARA BAADA YA KUFUNGA BARABARA KWA MASAA KADHAA ”
Post a Comment