Monday, May 26, 2014
MAJAMBAZI YAUA MFANYABIASHARA KWA RISASI NA KUPORA PESA HUKO SHINYANGA
Do you like this story?
Mfanyabiashara
mmoja aliyejulikana kwa jina Kulwa Cosmas(42) mkazi wa eneo la Ndala mjini
Shinyanga akiwa nyumbani ameuawa kwa kupigwa risasi moja ya shingoni
baada ya kuvamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi.
Tukio
hilo limetokea jana saa moja na nusu usiku katika eneo la Ndala mjini Shinyanga.
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi mwandamizi wa
polisi Evarist Mangalla amesema chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa.
Kamanda
Mangalla amesema tayari jeshi la polisi linawashikilia watu wanne kwa mahojiano
zaidi kuhusiana na tukio hilo.
Amewataja
watu hao kuwa ni Haudax James(36) mkazi wa Tambukareli mjini
Shinyanga,Pirima Gwiliza(43) mkazi wa Tambukareli mjini Shinyanga,Paulo
Masalu(31) mkazi wa Ngokolo mjini Shinyanga pamoja na Ramadhan Juma(45) mkazi
wa Kitangiri mjini Shinyanga .
Siku
hiyo hiyo ya jana mwanamme aitwaye Yahaya Mrisho(46)ambaye pia ni
mfanyabiashara mkazi wa kata ya Ibinzamata katika manispaa ya Shinyanga
amevamiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana wanaodhaniwa kuwa ni
majambazi wakiwa na silaha aina ya SMG kisha kumpora pesa taslimu
300,000/= ,vocha za simu zenye thamani ya shilingi 150,000/= pamoja na simu 4
za mkononi zisizojulikana thamani yake.
Kamanda
Mangalla amesema chanzo cha tukio hilo ni kuwania mali na kwamba mpaka sasa
hakuna mtu aliyeshiliwa na jeshi la polisi na ametoa wito kwa wananchi kutoa
taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa wahusika wa tukio hilo.
Na Kadama Malunde wa Malunde1 blog Shinyanga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAJAMBAZI YAUA MFANYABIASHARA KWA RISASI NA KUPORA PESA HUKO SHINYANGA”
Post a Comment