Monday, May 26, 2014

YULE BIBI ALIYEKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA UWANJA WA NDEGE DAR AANGUA KILIO MAHAKAMANI MPAKA HAKIMU AKAAHIRISHA KESI YAKE



Bibi wa Kinigeria, Olabisi Ibidun Cole akipelekwa mahakamani.



BIBI wa Kinigeria, Olabisi Ibidun Cole (65), leo ameangua kilio katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar ers Salaam wakati akipelekwa kizimbani kwa ajili ya kusomewa kesi yake ya kunaswa na madawa ya kulevya yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 37.

Hakimu aliyepelekewa kesi hiyo, Frank Mushi, aliiahirisha kesi hiyo mpaka kesho ili bibi huyo ambaye hajui Kiswahili wala Kiingereza atafute mkalimani.\

Cole alisema lugha anayoweza kuitumia kiufasaha ni Kiyoruba ambacho hutumiwa nchini Nigeria. Katika hali iliyoonesha kukata tamaa, bibi huyo alianza kuangua kilio akiomba Mungu amsaidie.

0 Responses to “YULE BIBI ALIYEKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA UWANJA WA NDEGE DAR AANGUA KILIO MAHAKAMANI MPAKA HAKIMU AKAAHIRISHA KESI YAKE”

Post a Comment

More to Read