Monday, May 26, 2014
MAAJABU: MAITI YATUMWA KWA NJIA YA POSTA KAMA BARUA...!!!!!
Do you like this story?
Polisi nchini Japan wanachunguza kisa
cha kushangaza ambapo maiti ya mwanamke aliyeuawa ilitumwa kutoka Osaka hadi
Tokyo kwa njia ya posta.
Inaaminika mwanamke huyo, Rika Okada,
alidungwa kisu na mwili wake kuwekwa ndani ya sanduku ambayo ilitiwa kibandiko
na karatasi iliyosema kuwa sanduku hiyo ilikuwa imemeba mwanasesere.
Sanduku hiyo, iligunduliwa ikiwa katika
sehemu ya kuhifadhi vitu katika kituo cha posta.
Polisi wanasema kuwa sehemu ambako
sanduku hiyo ilipatikana imewekwa, ilikuwa imekodishwa kwa kutumia kadi ya
benki ya mwanamke huyo.
Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo
alitoweka tangu mwishoni mwa mwezi Machi, alipotuma ujumbe wa mwisho kwenye
ukurasa wake wa Facebook kwamba alikuwa anaenda kukutana na rafiki yake wa muda
mrefu ambaye alikuwa hajamuona kwa miaka mingi.
Bbc
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAAJABU: MAITI YATUMWA KWA NJIA YA POSTA KAMA BARUA...!!!!!”
Post a Comment