Monday, May 26, 2014
KURA KUHESABIWA UPYA LEO MALAWIMALAWI
Do you like this story?
Nchini Malawi kura za uchaguzi mkuu zinatarajwa kuhesabiwa upya hii leo
katika maeneo ambapo imedhihirika kuwa idadi ya wapiga kura haiwiani na idadi
ya wale waliojiandikisha kupiga kura.
Uchaguzi
mkuu wa Malawi umezidi kuchukua sura mpya baada ya wanasiasa na wanasheria
nchini humo kupeleka malalamiko yao mahakamani, na kuzidi kuchelewesha matokeo
ya uchaguzi huo uliofanyika jumanne iliyopita.
Kulingana
na mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ya BBC aliye mjini Lilongwe, Baruan Muhuza,
hali nchini humo imekuwa ya sintofahamu ambapo hakuna ye yote anayejua uchaguzi
utaishia wapi.
Anasema
kuwa tume ya uchaguzi imekiri kuwa kuna maeneo kadhaa ambayo kuhesabu kwa kura
kutarudiwa kwa sababu kura zilizopigwa zinazidi waliojisajili.
"
Tume ya uchaguzi inasema kuwa kuna maeneo mengine ambako watu wamepiga kura
mara tatu au mara nne kama vile mji wa Mangochi waliosajiliwa ni watu 39,000
pekee lakini kura zilizopatikana hapo ni 180,000," Baruan alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KURA KUHESABIWA UPYA LEO MALAWIMALAWI”
Post a Comment