Monday, May 26, 2014
TAZAMA PICHA ZA VIJANA WA MBWA MWITU NA PANYA ROAD WALIOKAMATWA NA JESHI LA POLISI
Do you like this story?
Hawa ndio viongozi wa panya road na mbwa mwitu ambao tayari wameshakamatwa |
Jeshi la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanya msako wa nyumba kwa nyumba, mtaa
na maeneo yaliyoathirika kwa hofu ya vijana ambao ni vibaka maarufu kama Mbwa
mwitu au Panya Road. Msako huu uliofanyika ndani ya masaa 24 hadi
alfajiri ya tarehe 26/5/2014 kwa lengo la kuwaondolea hofu na uhalifu dhidi ya
makundi ya vijana wadogo wasio na ajira ambao uliibuka hivi karibuni.
Maeneo
yaliyoathirika ni Kigogo, Magomeni, Tabata, maeneo yote yanayozunguka mto
Msimbazi, maeneo ya Mbagala nk. Msako huu unaendelea kufanywa na askari
wa vikosi maalum ambao wamepewa kazi ya kuhakikisha kuwa vikundi hivyo
haviibuki tena na vinatokomezwaa kabisa kwa kuwakamata wale wote
wanaojihusisha na vitendo vya kuvamia kwa mkundi wananchi ambao hawana hatia
Kamishna kova ambaye amezungumza na wanahabari muda
mfupi uliopita
Kati ya
watuhumiwa 149 waliokamatwa mmoja amegundulika kuwa ni kiongozi aitwaye
ATHUMANI SAIDI miaka 20, Mkazi wa Kigogo na amekiri anaongoza kundi la watu
zaidi ya 15 ambao baadhi yao ni kati ya waliokamatwa.
Imegundulika
pia kwamba vijana hawa wanatumia dawa za kulevya aina ya bangi na wengine
hujichoma sindano na kuwafanya iwe rahisi kujihusisha na matukio ya
uhalifu. Vijana hao hupenda kushiriki katika ngoma kama Mnanda, Mchiriku,
Kigodoro, Kanga moja nk. ambazo kwa kawaida huchezwa hadi usiku wa manane.
Wakitoka
katika ngoma hizo hujikusanya pamoja na kufanya matukio ya uporaji kwa mtu
wanayekutana naye, kufanya uvunjaji katika majumba na wakati mwingine wana
mtindo wa kugema mafuta ya diesel au petrol katika matanki ya malori
yanayosafirisha mafuta.
Operesheni
kali inafanyika katika maficho ya wahalifu hao ikiwa ni pamoja na daraja la
River side, Kigogo darajani, Manzese, maeneo ya Tandale pamoja na maeneo
mengine ya maficho mkoa wa Kipolisi Temeke.
Tunawasiliana
na Maafisa utamaduni wa Wilaya zote za Mkoa wa D’Salaam kusimamisha utoaji wa
vibali wa ngoma za usiku ambazo hazina tija. Pia Jeshi la Polisi
linafuatilia na kuwavizia vijana wanaopora watu wanaotoka katika sherehe
za usiku kama vile Harusi na wanaotoka katika mikesha ya Ibada na sehemu zozote
zenye mikusanyiko.
Aidha Jeshi
la Polisi wanapambana na vijana wanaowavizia watu katika vituo vya mabasi pindi
wanapotoka alfajiri kwenda katika shughuli zao za kila siku.
Zipo taarifa
kwamba baadhi ya wazazi wasio waaminifu wamewasafirisha watoto wao wahalifu
katika makundi haya kwenda mikoani ili kukwepa wasinaswe na msako huu
mkali. Hata hivyo Jeshi la Polisi lina mtandao wa kutosha kati yake na
mikoa mingine na nchi jirani hivyo litawatafuta popote walipo na kuwakamata.
Oparesheni hii ni endelevu na ya kudumu hadi kero hii ya vibaka itakavyokwisha
kabisa. Baadhi ya majina waliokamatwa ni kama ifuatavyo:-
1. DANIEL PETER @ MALUNDE, miaka
25, mkazi wa Yombo Kigunga
2. MWISHEHE ADAM, miaka 35, mkazi
wa Mtoni mashine ya maji
3. MOHAMED SAID, miaka 32, mkazi
wa Mtoni
4. JAKAMA ALPHONCE, miaka 23,
mkazi wa Mtoni Kilakala
5. HAMADI MDUDU, miaka 25, mkazi
wa Mbagala
6. SALUM MUSA, miaka 25, mkazi wa
Kiwalani
7. ANTHONY DANIEL, miaka 20, mkazi
wa Mashine ya maji
8. FIDELIN ANTHONY, miaka 18,
mkazi wa Kigogo
9. HAMZA MAZUMA, miaka 19, mkazi
wa Kigogo
10.
MGANGA ABEID, miaka 20, mkazi wa Kigogo
11.
SAID ABEID, miaka 19, mkazi wa Kigogo
12.
SALUM NYENJE, miaka 36, mkazi wa Chamazi
13.
DOMINICK PETER miaka 22, Mkazi wa Kigogo
14.
KULWA ABEID, miaka 20, mkazi wa Mabibo
15.
MUSA IBTRAHIM, Miaka 20, mkazi wa Magomeni
16.
HUSSEIN SHABAN, miaka 22, Mkazi wa Magomeni
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAZAMA PICHA ZA VIJANA WA MBWA MWITU NA PANYA ROAD WALIOKAMATWA NA JESHI LA POLISI”
Post a Comment