Monday, May 26, 2014
MGOMO WA MADEREVA NA MAKONDAKTA WA DALADALA LEO ASUBUHI KUGOMA KUPELEKA ABIRIA MWENGE KUTOKA MAKUMBUSHO, DAMU YAMWAGIKA
Do you like this story?
Kamanda wa Polisi Kinondoni akiongea na waandishi wa habari kuelezea ni jinsi gani watashughulikia shida ya barabara hiyo ya kutoka kituoni makumbusho kuelekea mwenge |
Msururu wa daladala zikiwa ndani ya kituo cha makumbusho baada ya kugoma leo kuelekea mwenge kupeleka abiria |
Hapo ni Madereva na makondakta wakilikimbiza basi la UDA ambalo lilimkata mkono dereva mwenzao wakati wanalizuia lisiweze kutoka ndani ya kituo kuendelea na safari. |
Abiria wanaotumia njia ya makumbusho kuelekea Mwenge wakitokea Tandika na
Mbagala leo wameonja Joto ya jiwe kwa takribani masaa manne baada ya mabasi
yanayoptumia kituo cha ndani kugoma kupeleka abiria mwenge kutokana na ubovu wa
barabara za ndani wanazotumia kupita kuelekea kituo cha mwenge.
Sakata hilo
lilianza pale magari yalipofika kituo cha ndani cha makumbusho na kuwashusha
abiria wote na kugoma kuendelea na safari ya kuelekea mwenge,ndipo mzozo mkubwa
ulipozuka na kupelekea Sumatra na vyombo vya Usalama kufika eneo La Tukio na
kuweza kuongea na madereva hao,lakini madereva hao na makondakta waliendelea
kugoma mpaka pale walipohaidiwa kuwa ndani ya wiki moja barabara hizo zitakuwa
zimerekebishwa na kuwa nzuri,hivyo watumie njia kuu kuelekea mwenge.
PICHA NA HABARI NA DJ SEK BLOG
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MGOMO WA MADEREVA NA MAKONDAKTA WA DALADALA LEO ASUBUHI KUGOMA KUPELEKA ABIRIA MWENGE KUTOKA MAKUMBUSHO, DAMU YAMWAGIKA”
Post a Comment