Wednesday, April 2, 2014

KESI YA ZITTO YAZIDI KUPIGWA KALENDA.




Dar es salaam kesi ya aliyekuwa naibu katibu mkuu wa chadema zitto kabwe dhidi ya chama chake imepigwa kalenda  hadi mei 29 2014 .

Kesi hiyo ilipangwa kutajwa jana katika mahakama kuu kanda ya dare s salam jaji john utamwa  anayeisikiliza lakini iliahirishwa  na msajili wa wilaya ya  wa mahakama kuu kanda ya dar es salaam  amir msumi.

Akiahirisha kesi hiyo msumi alisema jaji utamwa  hakuweza kufika jana kwa sababu anaumwa na akapanga kesi hiyo itajwe  mahakamani  hapo tarehe hiyo.

Hii ni mar aya pili kwa kesi hiyo kuahirishwa  na wasajili kutokana na sababu za ugonjwa wa jaji  utamwa mara ya kwanza iliahirishwa  na msajili wiliam mtaki Februari 13 2014

Zitto ambaye pia ni mbunge wa kigoma kaskazini alifungua kesi h iyo dhidi ya bodi ya wadhamini wa chadema akiomba mahakama  hiyo ikizuie  chama kujadili uanachama  wake  hadi rufaa anayokusudia kuikata baraza kuu la chama kupinga kuvuliwa nyadhifa  itakaposikilizwa.

Katika kesi hiyo namba 1  ya 2014 zitto pia aliiomba mahakama hiyo imwamuru katibau mkuu  wa chadema mapatie mwenenod na taarifa  za kikao cha kamati kuu ya chadema kilichomvua  nyadhifa zote  alizokuwa  nazo ndani ya chama na iwazuie walalamikiwa  kumwingilia katika utekelezaji wa majukumu yake kama mbunge wa kigoma kaskazini

0 Responses to “KESI YA ZITTO YAZIDI KUPIGWA KALENDA.”

Post a Comment

More to Read