Wednesday, April 2, 2014

BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI LAVUNJIKA.




Bunge la afrika mashariki (Eala) likenza kuonekana  kufanana na bunge la katiba  linaloendelea mjini Dodoma.

Bunge hilo jana limevunjika bila kujulikana litakutana tena lini baada ya kuibuka mabishano  ya kisheria kuhusu hoja  ya kutokuwa na imani na spika Margret zziwa.

Hoja ya kumg’oa  spika zziwa ilianza kuzungumzwa kwenye  vyombo vya habari bya afrika mashriki kwa wiki kadhaa  sasa na hatimaye kuwasilishwa jana na mbunge peter mathuki kutoka kenye kwa niaba ya wenzake  shy rose bhanji  wa Tanzania, nyiranilimo Odette  wa Rwanda na hafsa mossi kutoka Burundi.

Awali bunge hilo linapaswa kuanza vikao vyake saa 8:00  mchana lilichelewa kaunza  hadi saa 9:44 alasiri baada ya wabunge wa kigoma kuingia ukumbini walipobani kuwa  hoja ya kumng’oa spika  haikuwa miongoni kwa shughuli za bunge kwenye kikao cha jana.

Hata hivyo dakika moja tangu mathuki alipanza kusoma maelezo ya hoja hiyo mbunge fred mukassa mbidde  aliinuka na kuomba mwongozo wa spika na alipopewa nafasi  alipinga hoja  hiyo kuwasilishwa  na kujadiliwaa na kujadiliwa kwa madai kuwa kuna kesi katika  mahakama  ya afrika mashariki (EACJ) inayohusiana na hoja hiyo.

Akifafanua mbidde alisema kesi hiyo inaomba mwongozo na ufafanuzi wa kisheria kuhusu  kanuni ya 9 ya bunge la EAC inayoelekeza  utaratibu  wa kumwondoa madarakani spika wa eala iwapo kutatokea  haja ya kufanya hivyo.

 Wakati mbunge  mbidde akiwa bado amesimama huku akiendelea  kutoa hoja yake mbunge joseph ombasa kutoka Kenya aliinuka na kumpinga  mbunge mwenzake aksiema nataka kulipotosha bunge kwani  kifungu 38 (3) kinaruhusu bunge hilo kujadili hoja yoyote yenye masilahi ya umma wa EAC ikiwamo hilo l a kumgoa spika.

Baada ya hoja ya ombassa mwanasheria wa EAC kaahwa alisimama kuto ufafanuzi  wa kisheria licha ya kukiri kuwapo kesi mahakamani  alisema tayari mahakama hiyo imetoa uamuzi mdogo kuw shauri  hiyo  imetoa  uamuzi mdogo kuwa shauri hiyo haliwezi kuzua shughuli na mjadala wowote wenye nia ya kumwondoa spika madarakani.

Hoja hiyo ya mwnasheria  ilimwibua tena mbunge mbidde  aliyehoji  kwanini maelezo ufafanuzi  kwa mwanasheria  huyo kutoa mwelekeo wa ulipo msimamo wake kuhusu hoja iliyokuwa mbele ya bunge.

0 Responses to “BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI LAVUNJIKA.”

Post a Comment

More to Read