Wednesday, June 4, 2014
POLISI WAONGEZWA MISHAHARA BRAZIL
Do you like this story?
![]() |
Polisi waliandamana wakitaka nyongeza ya mishahara |
![]() |
Maandamano ya polisi mjini Rio
|
Serikali
ya Brazil inapendekeza kuwapa nyongeza ya asilimia 15.8 mishahara polisi wake
ili wasigome wakati wa ufunguzi wa michuano ya kombe la dunia wiki ijayo.
Maafisa
wakuu wa polisi watapokea nyongeza ya asilimia 12 kuanzia mwezi Julai na
nyingine ya asilimia 3.8 mwezi Januari.
Makubaliano
hayo yanakuja baada ya mgomo wa polisi mapema mwaka huu ambapo takriban watu
250,000 walishiriki.
Maandalizi
ya kombe la dunia ambalo linaanza tarehe 12 Juni, yamekumbwa na maandamano ya
kupinga serikali kwa kutumia gharama kubwa kuandaa michuano hiyo.
Polisi
ambao hukabiliana na vitendo vya uhalifu na kupambana na ulanguzi wa madawa ya
kulevya pamoja na ugaidi, pia watahakikisha usalama mipakani na katika viwanja
vya ndege.
Chama
cha wafanyakazi kinachowawakilisha maafisa hao wa polisi, Fenapef, kimeelezea
kufurahishwa na hatua ya serikali kuwaongea mishahara kabla ya kuanza kwa
michuano ya kombe la dunia na kabla ya uchaguzi tarehe 5 Oktoba.
Mkuu
wa chama hicho alisema kuwa serikali pia imekubali kubuni kikundi cha
waakilishi watakaozungumzia swala la kuwapandishwa vyeo polisi waliofika
kiwango hicho.
Mwezi
jana polisi hao waligoma wakitaka kuongezwa mishahara katika majimbo 14 nchini
humo huku walimu na wafanyakazi wa umma pia wakidai mazingira bora ya kazi na
nyongeza ya mishahara.
Serikali
imeimarisha usalama katika maeneo yote 12 yatakayotumiwa kwa michuano hiyo huku
polisi 20,000 wakitarajiwa kudhbiti ulinzi mjini Rio.
Wadadisi
wanasema kuwa hatua ya serikali ni kutaka kuhakikisha kuwa maandamano
yaliyoshuhudiwa wakati wa kombe la mashirikisho mwaka jana hayatashuhudiwa tena
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “POLISI WAONGEZWA MISHAHARA BRAZIL”
Post a Comment