Wednesday, June 4, 2014
BRAZIL YATETEA MAANDALIZI YAKE.
Do you like this story?
![]() |
Rais Roussef ametetea vikali maandalizi ya kombe la dunia Brazil |
Rais
wa Brazil Dilma Rousseff ametetea jinsi ambavyo taifa lake limetayarisha Kombe
la Dunia litakaloanza juma lijalo jijini Sao Paulo.
Amesema
kuwa michezo hiyo itakuwa yenye ufanisi mkubwa ijapokuwa kumekuwepo na
kukosolewa kwa kuchelewa kwa nyanja na miundombinu mbalimbali.
Aliwaambia
wanahabari kuwa matatizo ya aina ile ni ya kawaida kila mahali.
Bi
Rousseff ambaye huenda akakumbwa na maandamano mapya ya kupinga serikali,
alisema kuwa hawataruhusiwa kuvuruga mashindano hayo.
''Kila
mahali duniani, miradi mikubwa ya uhandisi mara kwa mara hutatizika,” bi
Rousseff aliwaambia wanahabari kutoka katika mataifa ya kigeni katika makazi ya
rais jijini Brasilia.
Amesema
kuwa hakuna anayeweza kutengeneza reli za chini ya ardhi isipokuwa labda
Uchina.
Hayo
aliyasema kuhusu kuchelewa kwa miradi ya miundombinu, jambo ambalo limewakera
wananchi wengi wa Brazil waliotarajia kunufaika kutokana na kuboreswa kwa
miundombinu hiyo.
Mifumo
ya usafiri katika miji ya Cuiaba, Salvador, Recife na miji mingine mingi
haijakamilishwa kwa kuwa juhudi zote zilielekezwa katika kukamilika kwa nyanja
za kandanda zitakazotumika katika mashindano hayo.
Rais
huyo alitaja kuchelewa huko kama ''gharama ya demokrasia yetu.''
Akizungumzia
maandamano ya kupinga Kombe la Dunia la hivi majuzi- ambayo baadhi yaligeuka
kuwa vurugu- rais alisema kuwa ingawa maandamano yaliambatana na demokrasia,
maelfu ya polisi na askari zaidi watatumiwa kuhakikisha kuwa haitavuruga Kombe
la Dunia.
''Tunawahakikishia
watu wote usalama,” alisema.
Zaidi
ya watu milioni moja waliingia mitaani wakati wa michezo ya Confederation
kuandamana kupinga ufisadi na kile wanachodhani ni matumizi ya kupindukia
katika kutayarisha Kombe la Dunia.
Maandamano
hayo ambayo mwanzo yalianza kama makusanyiko madogo ya watu waliopinga
kuongezeka kwa naulikatika usafiri wa umma ulianza kuwa baada ya polisi kutumia
mbinu nzito kuwatawanya waandamanaji.
Bi
Rousseff alisema kuwa vikosi vya usalama vitafanya kazi kwa uangalifu wakati
huu.
Kikundi
kidogo chenye waandamanaji wanaopinga serikali kililenga mechi ya kirafiki
iliyokuwa ikichezwa baina ya Brazil na Panama katikati ya jiji la Goianiasiku
ya Jumanne.
Waandamanaji
hao waliokusanyika karibu na uwanja walikemea gharama kubwa ya michezo hiyo
huku wakisema kuwa pesa nyingi ingetumiwa kugharamia huduma za umma ili
kupunguza kukosekana kwa usawa.
Michezo
hiyo itaanza tarehe 12 mwezi Juni huku wenyeji Brazil wakichuana na Croatia
jijini Sao Paulo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BRAZIL YATETEA MAANDALIZI YAKE.”
Post a Comment