Tuesday, April 15, 2014

MILIONI 34 ZAPATIKANA MECHI YA AZAM FC NA MBEYA CITY FC.








JUMLA  ya shilingi milioni  34,070,000 zimepatikana katika mechi ya Mbeya City na Azam ya Jijini Dare es salaam  iliyochezwa April 13 mwaka huu  katika uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine huku timu  ya Azam ikiondoka na Ushindi wa goli 2-1.

Akisoma mapato hayo Katibu  wa chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA) Selemani Harubu , amesema kati mapato hayo shilingi milioni 7,628,074.99 zimeenda kwa kila timu.

Amesema, gharama ya Vat ni shilingi milioni  5,197.118.64  tiketi shilingi 3,015,000 gharama ya mchezo 2,327,209,305.32 huku  kamati ya ligi ikiondoka na shilingi 2,327,209.322.

Amesema,  TFF  imepata shilingi  1,163,604.66 na MREFA ikiondoka na shilingi 905,025,84 na uwanja ukipata shilingi 3,878,682.20.

Aidha katika Mchezo baadhi ya wadau mbalimbali wa mpira jijini mbeya wamedai kuwa ushindi huo wa Azam hakuwa sawa kwa madai kuwa mwamuzi wa mchezo huo Nathan Lazaro kutoka Kilimanjalo kuwa aliipa ushindi Azam kwa goli lisilo halali .

Aidha kufuatia matokeo hayo Azam wamejitawaza kuwa mabingwa wapya ligi kuu vodacom Tanzania Bara kwa kufikisha Pointi 59 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote huku ikibakiwa na mchezo mmoja mkononi .

0 Responses to “MILIONI 34 ZAPATIKANA MECHI YA AZAM FC NA MBEYA CITY FC.”

Post a Comment

More to Read