Tuesday, April 15, 2014

PRISON WAKIRI KUWA PETER MICHAEL AMECHANGIA TIMU KUWA PABAYA.




Licha ya kufunga mabao matano katika mzunguko wa pili wa ligi kuu, Tanzania,mshambuliaji wa timu ya soka ya Tanzania Prisons ametupiwa lawama kuwa kupoteza kwake nafasi za kufunga magoli kumechangia timu hiyo kuwa katika hatari ya
kushuka daraja.

” Peter ni mchezaji wetu, ni mfungaji wa kutegemewa katika timu lakini hatoi mchango wa kutosha. Anapoteza sana nafasi, kitu ambacho kimetugharimu katika michezo minne iliyopita”.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka ndani kabisa ya timu hiyo, Peter mwenye mabao tisa msimu huu ameambiwa anatakiwa kuongeza umakini uwanjani ili kuinusuru timu yake isishuke daraja.

” Mwalimu ameliona hilo na kumtaka apigane kuisaidia timu. Kazi yake ni kufunga magoli kitu ambacho ana uwezo nacho, ameambiwa kuongeza umakini na kutumia vizuri nafasi anazopata.

Ligi imekuwa ngumu lakini ni uzembe wetu wenyewe tuliofanya katika michezo ya hivi karibuni iliyopelea hali hii”.

0 Responses to “PRISON WAKIRI KUWA PETER MICHAEL AMECHANGIA TIMU KUWA PABAYA.”

Post a Comment

More to Read