Tuesday, April 15, 2014
SAMWEL SITTA ATUHUMIWA KUPENDELEA BAADHI YA WAJUMBE WA KATIBA .
Do you like this story?
MJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba,
Khamis Kigwangala, amemtuhumu Mwenyekiti wa bunge hilo, Samuel Sitta,
kuliendesha kwa upendeleo, uonevu na ushabiki.
Kigwangala alisema Sitta, amekuwa na
tabia ya kupendelea wachache huku akidai kufanya hivyo ni kutenda haki, jambo
ambalo si sahihi.
Kigwangala alitoa tuhuma hizo jana
asubuhi alipotaka mwongozo wa Mwenyekiti juu ya muda wa dakika 16 alizopewa
Msemaji wa wachache, Tundu Lissu, kumalizia hotuba yake iliyokatishwa wiki
iliyopita baada ya TBC kukatisha matangazo ya moja kwa moja.
Kigwangala alisema Lissu, alikuwa
amebakiza dakika mbili, lakini alishangazwa na uamuzi wa Sitta kuwa mjumbe huyo
amebakiza dakika 16.
“Mimi pia niliambiwa wakati nasoma hoja
ya kamati yangu, lakini TBC walikuwa wakikata matangazo lakini nilipokuandikia
kuhusu jambo hili hukunisikiliza, lakini kwa Lissu naona unafanya hivyo, sasa
unaona kuwapendelea wachache ndiyo kutenda haki?” alihoji.
Akijibu mwongozo huo, Sitta alisema
tuhuma hizo zimemsikitisha kwa kuwa mambo mengi anayoyafanya anategemea
wataalamu waliopo bungeni hapo.
“Nasikitika kutuhumiwa nafanya
upendeleo, mimi nategemea wataalamu wao ndiyo wanashika saa na wao ndiyo
wanasema umebaki muda fulani, mimi sitazami saa yangu na kuamua.
“Ikiwa hawa watatu wamekosea basi ni
bahati mbaya wao ndiyo wamesema hizo dakika 16 si mimi, ni kweli jana Jumapili,
uliniletea barua nyumbani kulalamikia kuhusu kutopewa nafasi kama Lissu,”
alisema.
Sitta alisema baada ya kuipata barua ya
Kigwangala alimpa maelekezo Katibu wa Bunge afuatilie TBC, kujua kama lina
ukweli ndani yake na baadae ilithibitika kuwa wakati wa Kigwangala akiwasilisha
maoni hakukuwa na tatizo la kukatika kwa matangazo.
“Jamani hili la Lissu halikuwa langu,
nilitahadharishwa na Mheshimiwa Freeman Mbowe, wote tukafuatilia tukabaini ni
kweli, sasa hili la Kigwangala, halikutolewa tahadhari,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ SAMWEL SITTA ATUHUMIWA KUPENDELEA BAADHI YA WAJUMBE WA KATIBA .”
Post a Comment