Wednesday, April 9, 2014
RAIS KIKWETE ACHAGULIWA KIONGOZI BORA AFRIKA.
Do you like this story?
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano
wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe akiongea na katika ubalozi wa Tanzania nchini Marekani mjini Washington DC, Marekani, ambako atapokea tuzo ya Africa’s
Most Impactful Leader of the Year kwa niaba ya Mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete, Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania mjini humo leo.
wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe akiongea na katika ubalozi wa Tanzania nchini Marekani mjini Washington DC, Marekani, ambako atapokea tuzo ya Africa’s
Most Impactful Leader of the Year kwa niaba ya Mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete, Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania mjini humo leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amechaguliwa
kuwa Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi katika Maendeleo Barani Afrika
kwa mwaka 2013 .
Heshima hiyo kwa Rais Kikwete imetolewa na jarida maarufu la
kimataifa la African Leadership Magazine Group na Tuzo la heshima hiyo
itatolewa jioni ya kesho, Jumatano, Aprili 9, 2014, katika sherehe
iliyopangwa kufanyika Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C ikiwa ni
pamoja na chakula cha jioni.
Tuzo hiyo itapokelewa kwa niaba ya Rais Kikwete na Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe, ambaye
tayari amewasili mjini Washington kwa sherehe hiyo kubwa.
Tuzo hiyo ya heshima kubwa hutolewa kwa viongozi wa Afrika ambao
hutoa mchango mkubwa zaidi wa kiuchumi na kijamii kila mwaka kwa watu wao
na limetolewa kwa Rais Kikwete kwa mwelekeo wake usiokuwa wa kawaida na
wenye mafanikio makubwa kwa masuala ya utawala bora.
Jarida hilo linasema kuwa ukweli wa hali hiyo bora ya utawala bora
chini ya uongozi wa Rais Kikwete umeendelea kumiminiwa
sifa kimataifa na leo umeifanya Tanzania kuwa nchi ya kuigwa mfano kama
kituo cha uhakika cha uwezeshaji kutokana na mageuzi makubwa yaliyofanywa
katika sera na mifumo ya uchumi.
Jarida hilo linasema kuwa Rais Kikwete alikuwa chaguo kubwa na la kwanza
la wasomaji wa Jarida hilo ambao walipiga kura kupitia njia mbali mbali za
mawasiliano za jarida hilo.
Linasema Jarida hilo, “Kuhusu maoni ya wasomaji wetu juu ya
kiongozi yupi wa Afrika ambaye ni hodari zaidi kwa maendeleo ya kiuchumi
na maendeleo, matokeo ya majibu ya swali hilo yamedhihirisha bila shaka
yoyote kuhusu nafasi ya Rais Kikwete katika uongozi wa nchi yake. Na
ushahidi uko kila mahali – ameweza kusimamia uchumi
ambao umekuwa kwa wastani wa asili mia saba kwa miaka yote ya uongozi
wake.”
Sherehe za kesho, miongoni mwa mambo mengine, zitaliwezesha
Jarida hilo kutangaza mafanikio ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais
Kikwete kwa Jumuia ya Kimataifa, ikiwa ni pamoja na Jumuia ya Kimataifa
ya Kibiashara, wanadiplomasia na taasisi nyingine zenye ushawishi mkubwa
katika medani za kimataifa na zenye makao yake katika Jiji la Washington
na maeneo ya
jirani.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
PICHA NA IKULU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RAIS KIKWETE ACHAGULIWA KIONGOZI BORA AFRIKA.”
Post a Comment