Monday, April 14, 2014
TAARIFA KAMILI YA AJALI YA HELKOPTA ILIYOMBEBA MAKAMU WA RAIS NA MAAFISA WENGINE WA SERIKALI.
Do you like this story?
Helikopta waliyokua wakisafiria Makamu
wa Rais Dr. Gharib Bilal, waziri wa ujenzi John Magufuli, Kamanda wa Polisi
kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Said Meck Sadick imepata ajali asubuhi wakati ikipaa kutoka uwanja wa ndege Dar
es salaam. (kwa mujibu wa mashuhuda)
Taarifa zilizotoka muda mfupi baadae
zimeeleza kupata majeruhi lakini hakuna yeyote aliepoteza maisha baada ya
Helikopta hiyo kuanguka wakati ikianza safari kuwapeleka viongozi hao
kutembelea maeneo yaliyoathirika na mafuriko.
Wote walitoka salama na majeraha
madogomadogo ambapo pia kwenye taarifa nyingine iliyotolewa na TBC, wameendelea
na ziara ya kutazama athari za maafuriko kwenye sehemu mbalimbali ikiwemo
Pwani.
Ajali hii ya Helikopta imetokea siku
moja baada ya ndege ya shirika la ndege la Kenya kubamiza chini na kuharibu
upande wa kulia wa bawa kutokana na ukungu mkubwa uliokuwepo kwenye uwanja wa
ndege Dar es salaam wakati ikitua kutokea Nairobi, hakuna aliepoteza maisha ila
waliojeruhiwa wakati wa kushuka kwa dharura kutoka kwenye ndege.
Taarifa kutoka kwa mmoja wa Waliokuwemo
kwenye Helikopta hii ya jeshi inasema wakati inapaa kwenye umbali wa kama futi
tano hivi kutoka uwanja wa ndege Dar es salaam, ilizidiwa na upepo ulioirudisha
nyuma na kuangukia paa kabla ya kutua chini.
Kilichofanyika ni watu waliokuwemo
kutoka nje harakaharaka kisha aliekua akiiendesha kufungua tenki la mafuta na
kumwaga mafuta yote alafu baada ya muda mfupi vikosi vya zimamoto vikaanza
kuipiga maji helikopta hiyo ili kuepusha mlipuko.
Unaambiwa kama ingekua ni majira ya
moto, helikopta hii ambayo ilikua inawapeleka kutazama maafuriko yaliyookana na
mvua Dar es salaam ingeweza kuwa kwenye hatari zaidi ya kulipuka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAARIFA KAMILI YA AJALI YA HELKOPTA ILIYOMBEBA MAKAMU WA RAIS NA MAAFISA WENGINE WA SERIKALI.”
Post a Comment