Monday, April 14, 2014

UPDATES:MKUU WA MKOA WA ARUSHA AZUNGUMZIA TUKIO LA BOMU KULIPUKA KWENYE BAA USIKU APRILI 13, 2014.





Usiku wa April 13 2014 kwenye baa iitwayo ‘Arusha night park’ iliyopo Mianzini Arusha ambayo siku zote ni miongoni mwa sehemu zinazokua na mkusanyiko wa watu wengi kuanzia jioni, limerushwa bomu wakati watu mbalimbali wakitazama mpira.

Blog hii imepata nafasi ya kuongea na mkuu wa mkoa wa Arusha ambae ni kiongozi wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ambae amethibitisha kwamba ni watu 15 wamejeruhiwa kwenye mlipuko huo.
Anasema wote wamepelekwa hospitali ambapo uchunguzi wa awali umeonyesha bomu hilo ni la kutengenezwa kwa mkono na mpaka sasa hajajulikana alietekeleza shambulio hilo.

Kwenye sentensi nyingine pia amesema hakuna aliepoteza maisha kwenye shambulio hilo ambalo uchunguzi wa awali umeshatoka, ila baadae itatoka taarifa rasmi pale uchunguzi kamili utakapokamilika.

0 Responses to “UPDATES:MKUU WA MKOA WA ARUSHA AZUNGUMZIA TUKIO LA BOMU KULIPUKA KWENYE BAA USIKU APRILI 13, 2014.”

Post a Comment

More to Read