Monday, April 14, 2014
ZIPO HAPA KAULI ZILIZOTOLEWA BUNGENI LEO NA TUNDU LISSU, WASSIRA, MTIKILA NA ISMAIL JUSSA.
Do you like this story?
Zifuatazo ni kauli zilizotolewa na
viongozi mbalimbali wa zile kamati kwenye bunge la katiba linaloendelea sasa
hivi hapa Dodoma ambapo viongozi hawa leo April 14 2014 wameendelea kuwasilisha
taarifa kutoka kwenye kamati zao,
Ni maoni ya pande mbili ambazo ni maoni
ya wengi ambao ndio wanaounga mkono serikali mbili alafu maoni ya wachache
ambao wanaunga mkono uwepo wa serikali tatu.
Tundu Lissu: ‘Nusu karne ya uongo
iishe, Tanganyika iliuwawa na amri za Mwalimu Nyerere na hakuwa na mamlaka
kisheria kuiua, hatujawahi kuwa nchi moja, habari ya Tanzania kuwa nchi moja
iliingizwa ktk katiba miaka 20 baada ya muungano, nchi hii ni haramu…. miaka 50
ya kudanganyana ikome, nchi hii inahitaji kuelezwa ukweli’
Mchungaji Mtikila: ‘tulijengwa kwenye
misingi ya uongo ndio maana Mungu alishindwa kubariki hii nchi yetu kwa miaka
50, uongo tuuondoe, swala la muungano lilikua utapeli wa kisiasa, tuurudie
ukweli kuhusu uhuru wa Watanganyika na Wazanzibari’
Mh Wassira: ‘Hati ya Muungano
ipo, naahidi kwa niaba ya Jamuhuri itawasilishwa kwa Mwenyekiti ndani ya siku
mbili zijazo, kama Wananchi wangetoa maoni kutaka kuvunja muungano, je tume
ingeyaleta? serikali 3 italeta mgongano’
Mh Wassira: ‘Katiba ya Znz ndio
itabakia kuwa sheria kuu kwa Znz kwa mambo yasiyokua ya muungano, tukiweka
serikali 3 hapa zikaweka masharti kuna watu watapata matatizo, itapunguzia
Wazanzibari fursa’
Ismail Jussa: ‘Hoja za historia
kwamba tulikua vipi haziwezi kulibakisha taifa katika mgando, ukiangalia katiba
ya muda ya mwaka 1965 inaendelea kuitambua Tanganyika na kuwepo makamu wawili
wa Rais’
Ismail Jussa: ‘Mkataba wa muungano
haukutoa mamlaka kwa chombo chochote kubadilisha kilichopo ndani, ajabu bunge
limefanya, tunapokua Znz tunasema mengine tukija huku tunaufyata, Wazanzibari
watatuhukumu’
Ismail Jussa: ‘Zanzibar tumeachwa
watupu, tumechoka na hatukubali tena, ktk mfumo wa serikali mbili Zanzibar
haitaweza kujisimamia kamwe, hatutakubali kuendelea nao’
Ismail Jussa: ‘Kama kuna nia njema
kwa nini kuna kufichaficha, mfano mwingine hai ni Rais wa Znz kuondolewa kuwa
makamu wa Rais’
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ZIPO HAPA KAULI ZILIZOTOLEWA BUNGENI LEO NA TUNDU LISSU, WASSIRA, MTIKILA NA ISMAIL JUSSA.”
Post a Comment