Monday, April 14, 2014
JEZI ZA RONAIDO ZAONGOZA KWA MAUZO.
Do you like this story?
Jumla
ya jezi milioni 1 za mchezaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ziliuzwa msimu
wa mwaka 2013/14 na kuzidi jezi za timu nzima ya Bayern Munich ambayo iliuza
jezi 880,000.
Ronaldo
hivi sasa ndiye anayeshikilia tuzo ya mchezaji bora duniani, pia bidhaa
mbalimbali zenye jina lake zinanunulika sana sehemu mbalimbali duniani.
Kwa
mujibu wa gazeti la Bild la Ujerumani, klabu za Real Madrid na Manchester
United ndiyo zilizoongoza baada ya kila moja kuuza jezi 1.4 milioni mwaka 2013,
lakini kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu mauzo ya Manchester United yaliongezeka.
Mwaka
huu jezi za wachezaji wa Real Madrid kila moja inauzwa Dola 76 za Kimarekani
wakati mwaka jana zilikuwa zikiuzwa Dola 84 za Kimarekani (Dola 1= Sh1,620).
Gazeti
hilo pia lilitaja wachezaji ambao wameziwezesha klabu zao kuuza jezi nyingi
kuwa ni Real Madrid (Ronaldo, Bale, Xabi, Alonso), Man United (Rooney, van
Persie, Mata), Barca (Messi, Neymar, Xavi), Chelsea (Hazard, Oscar, Lampard),
Bayern (Ribery, Lahm, Schweinsteiger, Liverpool (Suarez, Coutinho, Sturridge),
Arsenal (Ozil, Wilshere, Ramsey), Juventus (Pirlo, Pogba, Tevez), Inter Milan
(Zanetti, Palacio, Nagatomo), AC Milan (Kaka na Mario Balotelli).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JEZI ZA RONAIDO ZAONGOZA KWA MAUZO.”
Post a Comment