Wednesday, May 14, 2014
NIKKI WA PILI ASIMULIA YALIYOMKUTA MAISHANI MWAKE, STORI KAMILI IPO HAPA
Do you like this story?
Drake
anasema ‘We started from the Bottom’ lakini Mweusi Nick wa Pili anasema
‘Haikuwa Rahisi’.
Nick wa
Pili ambaye ni moja kati ya rappers bora zaidi Tanzania na mshindi wa tuzo ya
KTMA ameelezea jinsi alivyohangaika wakati akiwa shule ya msingi katika maisha
ya kawaida ambayo wapo watanzania wengi wanayoyaishi hadi hivi sasa.
Akizungumza
katika kipindi cha The Jump Off ambapo yeye ndiye Mkali wa The Jump Off wa Wiki
hii anayesimulia story ya maisha yake ambayo ni somo tosha kwa vijana ambao
wanahangaika kutafuta, rapper huyo ameeleza jinsi alivyofanya shughuli ya kuuza
sambusa akiwa darasa la tatu hadi darasa la saba kila anapotoka shuleni saa nne
usiku huku akiwasaka wateja kokote walipo..
“Mimi maisha yangu niliyopitia unajua sio kama watu wanavyonidhania,
mimi nimepitia a very hard life. Mimi kuanzia nikiwa darasa la tatu nilikuwa
nauza sambusa.
"Nilikuwa natembeza kwenye nyumba za gongo, banana, mabaa na
nilikuwa nauza kuanzia saa kumi hadi saa nne usiku, niko darasa la tatu nimeuza
mpaka darasa la saba.
"Kwa hiyo watu wanapotuona Nick wa Pili… it’s not easy. Nafikiri
kama ukipata kusikiliza albam ya Chindo kuna ngoma inaitwa ‘Haikuwa Rahisi’
nilijaribu kuweka historia yangu pale..ilikuwa ngumu.”
Nick wa
Pili ambaye ni mdogo wake Joh Makini, ameeleza kuwa hata alipomaliza darasa la
saba kuingia sekondari ilikuwa ngumu kutokana na kikwazo cha fedha.
Ilimbidi
akae nyumbani miezi miwili akitafuta shilingi 20,000 za karo. Bahati nzuri
rapper huyo alizipata fedha hizo na alipoingia shule alikuta tangazo la mtihani
wa kumaliza muhula na alipoufanya alishika nafasi ya pili kutoka mwisho.
Kutokata
tamaa na kukaza ndiko kumempa nafasi ya kung’aa na kupata shahada ya uzamili
(masters) na kufanya vizuri kwenye muziki hadi sasa.
“Kwa hiyo
ndio life tuliyopitia, lakini if you put a struggle in everything…it’s
possible.”
Nick
anaachia wimbo wake alioupa jina la ‘Staki Kazi’ akiwa amewashirikisha G-Nako
na Ben Pol.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “NIKKI WA PILI ASIMULIA YALIYOMKUTA MAISHANI MWAKE, STORI KAMILI IPO HAPA”
Post a Comment