Wednesday, May 14, 2014
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA,ATAKAYEKACHA MAFUNZO JKT KUSHITAKIWA
Do you like this story?
Vijana
wasiopungua 45,000 watakaomaliza kidato cha sita watajiunga na Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria na watakaokwepa mafunzo hayo ya miezi mitatu,
watashtakiwa.
Mpango
huo wa kupitisha JKT wahitimu wa kidato cha sita na vyuo, ambao ulifutwa
mwanzoni mwa miaka ya 90 kutokana na matatizo ya kifedha na kurejeshwa bila
mafanikio ya miaka ya hivi karibuni, ulilenga kujenga uzalendo kwa vijana na
kuongeza ukakamavu.
Jana
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga, Dk Hussein Mwinyi alisema utaratibu huo
ni wa kisheria na si hiari, hivyo wahitimu wa kidato cha sita watambue kuwa ni
kosa kukaidi wito wa kujiunga na JKT.
Dk
Mwinyi, aliyekuwa anawasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya
wizara yake, alisema katika mwaka wa fedha 2014/2015, vijana watakaojiunga na
jeshi watafanya hivyo kwa awamu tatu.
Alisema
awamu ya kwanza itahusisha vijana 20,000 ambao wataingia katika mafunzo hayo
Juni hadi Septemba 2014 na kufuatiwa na wa awamu ya pili itakayochukua vijana
14,450 kuanzia Oktoba hadi Januari 2015 wakati awamu ya tatu ya vijana 10,550
itaanza Januari hadi Aprili 2015.
Hata
hivyo, kumekuwepo na mwingiliano wa muda wa kujiunga na jeshi hilo na wa
kujiunga na masomo ya juu. Kati ya vijana 15,000 waliotakiwa kujiunga na jeshi
hilo kati ya Oktoba 2013 na Januari 2014, waliojiunga walikuwa 1,002 tu.
Alipoulizwa
kuhusu mwingiliano huo, naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenister
Mhagama alisema atatoa ufafanuzi huo leo.
Akichangia
mjadala wa bajeti hiyo, mbunge wa viti maalumu (CCM), Esther Bulaya alitaka
mafunzo ya JKT kwa wabunge yafanyike kwa miezi miwili hadi mitatu badala ya
wiki mbili.
Bulaya,
ambaye alipitia mafunzo hayo pamoja na wabunge wenzake wakati mpango huo
uliporejeshwa mapema mwaka jana, alisema kuwa hali hiyo itawafanya wabunge hao
kujifunza mambo mengi zaidi.
Bulaya
aliwataja baadhi ya wabunge vijana wanaotakiwa kujiunga na mafunzo hayo kuwa ni
John Mnyika (Chadema-Ubungo) na Catherine Magige (viti maalumu-CCM).
“Mheshimiwa
Spika naomba uwaruhusu wabunge kwenda kwenye mafunzo kwa miezi miwili hadi
mitatu,” alisema na Bulaya na kuongeza:
“Katika
kambi za JKT kuna tatizo la vifaa vya afya, hivyo wizara iliangalie hilo ili
wanaokwenda katika mafunzo hayo wapate tiba sahihi na kwa wakati.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA,ATAKAYEKACHA MAFUNZO JKT KUSHITAKIWA”
Post a Comment