Sunday, May 25, 2014

POLISI WAWAKAMATA VINARA WA MBWA MWITU NA PANYA ROAD




JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata viongozi sita wa makundi ya uhalifu maarufu kwa majina ya Mbwa Mwitu na Panya Road.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi wa kanda hiyo, Suleiman Kova, aliwataja viongozi hao kuwa ni Athumani Said (20), Joseph Ponela, Clement Petter (25) na Romans Vitus (18) wakazi wa Kigogo.

Wengine ni Mwinshehe Adamu (37) mkazi wa Temeke na Daniel Petter (25) mkazi wa Yombo, huku kamanda huyo akibainisha kwamba maeneo yenye vijana hao wahalifu ni Kigogo, Magomeni, Tabata, Manzese na Mbagala ambapo askari wa kutosha wapo kwa lengo la kuwadhibiti.

Kova aliwaonya wanaoeneza uzushi kwamba makundi hayo ya wahalifu yamevamia maeneo hayo jambo alilodai kuwakosesha wananchi amani huku akisisitiza kuwa si kweli.

Amesema uchunguzi wa jeshi hilo umebaini kwamba chanzo cha uvumi huo ni baada ya mauaji ya vibaka wawili walihusishwa na makundi hayo yaliyotokea Mei 18 na Mei 20 mwaka huu eneo la Kigogo Sambusa.

0 Responses to “ POLISI WAWAKAMATA VINARA WA MBWA MWITU NA PANYA ROAD ”

Post a Comment

More to Read