Thursday, June 5, 2014
ADHABU KWA MKE KUMTELEKEZA MUME.
Do you like this story?
Mwanamke
mmoja nchini Kenya ameamrishwa na mahakama kumlipa mumewe shilingi elfu tatu au
dola 35 kama hela za kukidhi mahitaji yake na watoto wake kila mwezi.
Mwanamke
huyo kwa jina Roselyn Muyonga, ambaye anatuhumiwa kwa kuwatelekeza mumewe na
watoto wake watatu , huenda akafungwa miezi mitano jela au kutozwa faini ya
shilingi laki mbili ikiwa atakosa kutekeleza amri ya mahakama.
Afisaa
mmoja wa watoto katika jimbo la Kakamega Magharibi mwa Kenya, alisema kuwa
mwanamke huyo alipuuza jukumu lake la kulea watoto wake baada ya yeye na mumewe
kutalakiana.
Afisa
huyo alisema kuwa wanaume huachiwa majukumu mengi sana wakati wanapoachwa na
watoto na kwamba wanawake kama Roselyn wanapaswa kuamrishwa kuwatunza watoto
wao hata kama wameachana na waume zao.
Tayari
mashirika kadhaa yanataka kushinikiza sheria ya kuwashurutisha wanawake kutoa
mchango kwa kuwalea watoto wao wanapoachana na mwanamume au baba ya watoto.
Kwa
mujibu wa afisaa mmoja wa watoto, visa vya wanawake kuwatelekeza watoto wao
katika jimbo hilo vimeongezeka
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “ADHABU KWA MKE KUMTELEKEZA MUME.”
Post a Comment