Thursday, June 5, 2014
VIWANGO FIFA: BRAZIL YAJONGEA TARATIBU KATIKA NAFASI YAKE, TANZANIA NAYO YAJITUTUMUA.
Do you like this story?
BRAZIL
imekwea mpaka katika nafasi ya tatu katika viwango vya ubora duniani ikiwa ni
vya mwisho kabla ya michuano ya Kombe la Dunia haijaanza kutimua
vumbi. Katika viwango hivyo vya kila mwezi ambavyo hutolewa na Shirikisho
la Soka Duniani-FIFA Tanzania imekwea kwa nafasi tisa mpaka katika nafasi ya
113 na kuwazidi majirani zao Rwanda walioko katika nafasi ya 116. Nafasi
ya kwanza na pili katika orodha hizo imebaki kwa nchi za Hispania na Ujerumani
huku nafasi ya nne na tano ikishikiliwa na Ureno na Argentina. Kwa upande
wa Afrika Algeria kwasasa ndio wanaongoza wakiwa katika nafasi ya 22 baada ya
kuipita Ivory Coast walioporomoka mpaka nafasi ya 23 wakifuatiwa na Misri
waliopo katika nafasi ya 36. Wengine ni Ghana ambao wako katika nafasi ya
37 huku tano bora kwa upande wa Afrika ikifungwa na Cape Verde waliopo nafasi
ya 39.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “VIWANGO FIFA: BRAZIL YAJONGEA TARATIBU KATIKA NAFASI YAKE, TANZANIA NAYO YAJITUTUMUA. ”
Post a Comment