Thursday, June 5, 2014

MKATABA MNONO WA MILIONI 360 ZA BINSLUM KUINOGESHA MBEYA CITY.



Wakuu wa idara mbalimbali wa halimashauri ya jiji la Mbeya  wakiwa wanashuhudia tukio zima la kuweka saini katika Mkataba



Mkurugenzi wa kampuni ya Bin Slum Tyre Company Limited Bw Mohamed Ahmed Binslum akiweka saini Mkataba

Mwanasheria wa jiji akiwa anaweka saini katika mkataba




Waandishi wa Habari wakichukua tukio zima la kusaini Mkataba

Hatimaye  Timu ya Mbeya City  inayomilikiwa na Halmasahuri ya jiji la Mbeya ambayo inashiriki ligi Tanzania bara leo imewka saini katika mkataba mnono kwa ajili ya kudhamni Clabu hiyo  wa sh.milioni 360 kwa miaka miwili kutoka kampuni ya Binslum ya  Jijini Dar es salaam.

Mbeya City iliyojizolea sifa lukuki kwa mtindo wake wa kuzizidi timu zote zilizocheza ligi Kuu msimu uliopita imewashawishi wadhamini hao kuwekeza kwa timu hiyo kwa nia ya kuongeza chachu kwa timu za mikoani zinazocheza Ligi Kuu.
Akizungumza wakati wa kuweka saini mkataba huo katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji leo asubuhi, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Mohamed Binslum amesema udhamini wao umelenga kuleta changamoto na hamasa kwa timu za mikoani.

Binslum amesema kuwa wameamua kuwekeza kwa Timu ya Mbeya City kutokana na namna ambavyo timu hiyo imeonesha mtindo wa kipekee wa ushawishi kwa soka hapa nchini kinyume na ilivyozoeleka kwa timu kubwa za Yanga na Simba.

Alisema kuwa kampuni ya Binslum inaamini itanufaika kwa kutangaza bidhaa zake kupitia jezi za timu hiyo katika michezo yake kwa msimu wa mwaka 2015-16 na kuwa wamefikia makubaliano hayo na uongozi wa Mbeya City kutokana na mwitikio mkubwa wa wapenzi wa soka katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Awali akizungumza katika hafla hiyo fupi ya utiaji saini mkataba na kampuni hiyo Meneja Mbeya City Emmanuel Kimbe amesema kuwa anaamini ufadhili huo utachangia kuiongezea uwezo timu hiyo katika ligi Kuu msimu ujao wa 2015 na 2016.

Amesema kuwa mkataba huo utachangia kuongeza kipato cha timu hiyo na kuiwezesha kujikimu kwa matatizo madogo madogo ambayo anaamini yatatatuliwa kwa ufadhili huo wa miaka miwili.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya ambaye ndiye mmiliki wa timu hiyo Dkt. Samwel Lazaro amesema kuwa ufadhili kwa timu za mikoani utachangia klabu nyingi zisizo na uwezo wa kifedha kushiriki ligi kwa ushindani katika ligi na kukua kwa soka la Tanzania.

0 Responses to “MKATABA MNONO WA MILIONI 360 ZA BINSLUM KUINOGESHA MBEYA CITY.”

Post a Comment

More to Read