Thursday, June 5, 2014

MISS MBEYA 2014 KUPATIKANA KESHO.


Mratibu wa Miss Mbeya Bi, Amani Mbilo

Pichani ni warembo waliowahi kushiri shindano hilo picha na maktaba

Maandalizi ya shindano la  kumtafuta Miss Mbeya kwa mwaka 2014 yamefikia katika hatua za mwisho ambapo kesho June 6 mwaka huu  mrembo huyo  anatarajiwa kupatikana katika viwanja  City Pub, ambapo warembo 11 watachuana jukwaani kuwania taji hilo.



Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mbeya  Mratibu wa shindano hilo lililoandaliwa na kampuni ya Bomba Fm Radio, Amani Mbilo, alisema mshindi katika kinyang’anyiro hicho atazawadiwa kiasi cha shilingi 500,000.



Amesema mshindi wa pili atapata kiasi cha shilingi 300,000, mshindi wa pili 200,000, huku washiriki wote waliobaki wataambulia kifuta jasho cha fedha kama gharama ya usafiri wa kufika katika mashindano hayo.



“Washiriki hawa 11 ni kutoka katika wilaya mbili tu za Mbeya City Centre na Mbeya Vijijini  kutokana na wilaya nyingine kukosa hamasa ya kuendesha mashindano haya hali iliyosababisha ushiriki uwe wa wilaya mbili tu” alisema Mbilo.



Mratibu huyo aliwataja washiriki hao 11 kuwa ni Meryam Cephas, Juliana Gilbert, Joanitha Tibenderana, Matilda Hillu, Joyce Lameck.

Aliwataja washiriki wengine kuwa  ni Pendo Nelson, Atukuzwe Fabian, Anitha Patrick, Rhoda Joseph, Felister Godion na Emiliana Abdalah.

Wadhamini katika shindano hilo ni Tbl kupitia kinywaji cha Reds, Access Computer, Mbeya Peak Hotel, Kihumbe, Air Tanzania na Dorcus Saloon.



Aidha, Mbilo alisema katika shindano hilo litasindikizwa na burudani ya bendi ya muziki wa dansi nchini la Fm Academia kutoka Jijini Dar es salaa na mgeni rasmi ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi.

0 Responses to “MISS MBEYA 2014 KUPATIKANA KESHO.”

Post a Comment

More to Read