Thursday, June 5, 2014
USHER RAYMOND NA TYGA WALIVYOZAMA KWA CHRIS BROWN.
Do you like this story?
KutokaGerezani Kwa Chris
Brown kumekuwa Ni kitu cha Kufuatiliwa Sana, ili kufahamu ni Mchakato gani
ambao unaendelea kwa hivi sasa, ila Kitengo kisicholala cha Chimbua Chimbua,,
kimeshusha Ripoti yake ya Kwanza kama ambavyo TTM tunaishusha kwako Pia.
Breezy alipata Ugeni wa Kwanza wa
kimya Kimya kutoka Kwa marafiki zake, Usher Raymond na rapper Tyga akiwakilisha
Kundi la YMCMB, Jumanne ya Wiki Hii, katika maskani yake ya ENCINO, CALIFONIA.
Aidha baada ya kufika Nyumbani
kwa Breezy, inasemekana kuwa watatu hao walitumia Muda mwingi kupiga Stori za
hapa na pale, huku wakienjoy Mchezo wa basket ball ama Mpira wa Kikapu hapo
hapo maskani kwa Chris Brown.
Kama Ulikuwa hufahamu vizuri,
Tyga na Chris Brown wameshirikiana katika Mikwaju kadhaa ikiwemo DEUCES, HOLLA
AT ME, na Loyal ambayo inafanya Vizuri sana katika Soko la Muziki nna Media
Mbali mbali hapa Ulimwenguni.
Tofauti na Tyga, Usher Raymond
alitangaza awali kuwa, anashirikiana na Chris Breezy katika Albam yake Mpya
ambayo itaingia Sokoni Pindi itakapokuwa Tayari
Chris Breezy ametumikia Siku 108
Jela kati ya Siku 131 tangia March 24 Mwaka Huu, ambazo alihukumiwa kwa
Makosa kadhaa ikiwemo kukiuka Adhabu alizokuwa amepewa na mahakama Dhidi ya
makosa mbali mbali likiwemo lile la kuswapua makofi Ex-baby wake Rihanna
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)



0 Responses to “USHER RAYMOND NA TYGA WALIVYOZAMA KWA CHRIS BROWN.”
Post a Comment