Wednesday, June 18, 2014

BOMU LAONEKANA MTWARA, PICHA NA MAELEZO YAKE VIKO HAPA






Hili ni bomu ambalo jioni ya June 16 2014 kwenye kijiji cha Mdui kata ya Mawala wilaya ya Mtwara vijijini kwenye mkoa wa mtwara liliokotwa na watoto waliokuwa wakicheza karibu na eneo la makaburi.

Taarifa ilitolewa Polisi baadaye ambapo baada ya wataalamu kuja na kuchunguza waligundua ni bomu la kurusha kwa mkono ambalo lina namba TNT MORTAR BOMB 60MM,LOT SOL 618 ambapo Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi walichukua hatua za kiusalama na kwenda kulilipua porini.

Kaimu kamanda wa Polisi Mtwara Maisha Maganga alikuwa  na  haya  ya  kusema  kuhusiana  na  bomu  hilo:
"Ukiliangalia ni bomu ambalo ni la muda mrefu nadhani ni kipindi kile cha vita ya Msumbiji, tulilipeleka porini likalipuliwa na ulipuaji wake haukuwa na madhara… na sio kwamba ni bomu tunaweza kusema limeletwa ama imekuaje, ni bomu la muda mrefu tu"

0 Responses to “BOMU LAONEKANA MTWARA, PICHA NA MAELEZO YAKE VIKO HAPA ”

Post a Comment

More to Read