Wednesday, June 18, 2014
MWANAMKE AJIFUNGUA MTOTO WA AJABU MKOANI SINGIDA....HAKUHUDHURIA KLINIKI TANGU ABEBE MIMBA
Do you like this story?
Mwanamke
mmoja mkazi wa Kintinku, Wilayani Manyoni
mkoani Singida amejikuta akimwaga machozi
baada ya kujifungua mtoto mwenye kichwa
cha ajabu ( tepe tepe).
Tukio hilo limetokea jana asubuhi katika hospitali ya Kintinku Health Center iliyopo Wilayani Manyoni.....
Tukio hilo limetokea jana asubuhi katika hospitali ya Kintinku Health Center iliyopo Wilayani Manyoni.....
Akiongea kwa sharti
la kutotajwa jina lake kwa madai kuwa
yeye si msemaji wa hospitali hiyo,
Mkunga mmoja wa hospitali hiyo amedai
kuwa mama huyo alifikishwa hospitalini hapo
akiwa katika hatua za mwisho kujifungua.
"Alifikishwa
hapa akiwa katika hatua za mwisho
. Hakuwa na kadi yoyote ya Clinic
kwa kuwa hakuwahi kuhudhuria Clinic tangu
abebe mimba hiyo.
"Pamoja
na kutokuwa na kadi ya Clinic, tulianza
kumsaidia kujifungua, lakini mtoto aliyezaliwa
alikuwa ni wa tofauti kidogo na
alikuwa amefariki dunia.Kichwa chake kilikuwa
tepetepe na kimebonyea bonyea.
"Ilikuwa
ni ngumu kwetu kutambua tatizo alilokuwa
nalo mama huyo kwa kuwa hakuwa na
kadi yoyote ya Clinic ambayo ingeweza
kutusaidia kujua maendeleo ya mtoto huyo
alipokuwa tumboni ", alisema
Mkunga huyo.
Mpekuzi ilifanya
mahojiano na mama huyo ambaye naye
alionyesha kushangazwa na tukio hilo na
kusema hajui tatizo lililomfanya ajifungue mtoto
huyo kwa kuwa hakuwahi kusikia maumivu
ya aina yoyote wakati wa ujauzito huo
hadi alipofikia hatua ya kujifungua....
Katika mahojiano hayo,
mama huyo alisema kuwa huo ni uzao
wake wa 6 na hajawahi hudhuria Clinic
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWANAMKE AJIFUNGUA MTOTO WA AJABU MKOANI SINGIDA....HAKUHUDHURIA KLINIKI TANGU ABEBE MIMBA ”
Post a Comment