Thursday, June 12, 2014

CRISTIANO RONALDO NA WACHEZAJI WENZAKE KILA MTU AMEPEWA CHUMBA CHAKE, ARGENTINA WAWILI WAWILI


Chumba cha kulala: Nyota wa Ureno, Joao Moutinho ameposti picha hii kwenye mtandao wa Twita akionesha chumba chake cha kulala nchini Brazil.


WAKATI kitu cha kwanza atakachokiona Lionel Messi kila aamuka asubuhi ni mchezaji mwenzake Sergio Aguero baada ya wawili hao kupangiwa chumba kimoja cha kulala, Cristiano Ronaldo kwake ni tofauti kwani ataishia kuiona picha yake  kufuatia kupewa chumba cha peke yake.

Pengine hili litakuwa jambo jema kwa Ronaldo aliyeshangilia bao la nne la Real Madrid kwenye fainali ya UEFA baina ya Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid kwa kuvua jezi yake na kutunisha kifua chake.

Ureno waliwasili katika kambi yao na kukuta wameshaandaliwa vyumba vya kulala vikiwa na majina ya wachezaji na kikosi kwenye vitanda vyao, pia kumewekwa picha zao ukutani.

Kiungo Joao Moutinho na beki Joao Pereira wote kwa pamoja wameposti picha za vyumba vyao kwenye mtandao wa Twita na Instagram wakifurahia kabla ya kucheza mchezo wao wa ufunguzi wa kundi D dhidi ya Ujerumani mjini Salvador juni 16.
 Licha ya wasiwasi uliotanda juu ya Ronaldo kukivaa kikosi cha Joachim Low baada ya kusumbuliwa na majeruhi ya mguu aliyoipata kwenye mechi za UEFA, nyota huyo mwenye miaka 29 ameonekana kuimarika hasa baada ya kucheza kwa dakika 66 kwenye ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Ireland siku ya jumatano.
Baada ya mechi ya Ujerumani, vijana wa Paulo Bento watakabiliana na Marekani juni 22 mjini Manaus, kabla ya kucheza mechi ya mwisho ya makundi mjini Brasilia dhidi ya Ghana juni 26.
Hoteli ya Argentina kwenye kombe la dunia ilipangwa mapema wiki hii, huku ikionesha wachezaji gani watakuwa wanalala chumba kimoja wakati wote wa mashindano.

 Mpangilio unaonesha kuwa washambuliaji Messi na Aguero watakuwa wanalala chumba kimoja.

0 Responses to “CRISTIANO RONALDO NA WACHEZAJI WENZAKE KILA MTU AMEPEWA CHUMBA CHAKE, ARGENTINA WAWILI WAWILI”

Post a Comment

More to Read