Friday, June 13, 2014
SHEHENA YA VIROBA, VIPODOZI NA VYAKULA VILIVYOKWISHA MUDA WA MATUMIZI VYATEKETEZWA MKOANI MBEYA
Do you like this story?
Mamlaka ya
Chakula na Dawa kwa kushirikiana na uongozi wa wilaya za Rungwe na kyela
wamefanikiwa kukamata na kuteketeza shehena kubwa ya pombe haramu aina ya
viroba, vipodozi, dawa na vyakula ambavyo muda wake wa matumizi umepita,
bidhaa ambazo zimekamatwa wakati wa operesheni ya kutokomeza uingizwaji wa
pombe haramu za viroba mkoani mbeya.
Shehena ya
pombe haramu za viroba, vipodozi, vyakula na dawa ambazo muda wake wa matumizi
umekwisha vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 vimeteketezwa kwa
nyakati tofauti katika wilaya za rungwe na kyela, zoezi ambalo limesimamiwa na
kamati za ulinzi na usalama za wilaya hizo.
Mkuu wa idara
ya usafi na mazingira wilayani rungwe Dk. Nimroud kipoza na afisa wa mamlaka ya
mapato TRA wilayani kyela Paul Walalaze wanaelezea madhara ya bishaa hizo
kiafya na kiuchumi kwa watanzania.
Baadhi ya
vijana ambao wameunda kikundi cha kupambana na pombe haramu za viroba pamoja na
dawa za kulevya katika mpaka wa kasumulu wilayani kyela wamesema mafanikio yao
katika kudhibiti bidhaa hizo yanatokana na kupata ushirikiano mzuri kutoka
serikalini.
Meneja wa
mamlaka ya udhibiti wa chakula na dawa (TFDA) kanda ya nyanda za juu kusini,
Rodney Alananga amesema zoezi la kupambana na bidhaa hizo ni endelevu, hivyo
akawataka wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo kuacha ili kuepuka kupata
hasara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SHEHENA YA VIROBA, VIPODOZI NA VYAKULA VILIVYOKWISHA MUDA WA MATUMIZI VYATEKETEZWA MKOANI MBEYA ”
Post a Comment