Sunday, January 31, 2016

ONGEZEKO LA BAJETI KATIKA SEKTA YA UTALII




Katika mipango ya kukuza uchumi,  sekta ya utalii chini ya Prof Jumanne Maghembe ambaye ni Waziri mpya wa Maliasili na Utalii imeamua kuanza kuweka mikakati katika kuongeza bajeti ya kutosha kwa mwaka 2016,  ili kuongeza bidhaa na huduma zenye ubora kwa lengo la kuvutia watalii wengi zaidi nchini.

Sekta ya utalii imekuwa na mpango wa kuongeza watalii wa kigeni zaidi ya Million 3 mpaka kufikia 2018, ambapo mkakati huu utaenda sambambana na ongezeko la pato la taifa kuongezeka mara mbili ya kinachopatikana kwa sasa.

kwa upande wake mdau wa masuala ya Utalii, Bw. Andrea Guzzoni, Meneja mkazi wa JovagoTanzania alifafanua kuwa sekta ya utalii imekuwa mstari wa mbele katika kukuza uchumi baada ya kilimo, hivyo kama suala hili litatiliwa mkazo basi tunasubiria Tanzania mpya katika uchumi.

Aliendelea kwa kufafanua kuwa, “Sekta hii inabidi ikabiliane na matatizo yanayoikabili katika ukusanyaji wa kodi, kwa namna moja au nyingine inaweza kuwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo kama hatuta chukua hatua yeyote”.

“Hata hivyo,inabidi tuangalie maboresho katika nyanja tofauti tofauti, bado kuna wahudumu wasio na ujuzi wa kutosha, ukilinganisha na huduma ukiwa nje ya nchi na hapa ni tofauti, hivyo tujaribu kuweka mafunzo ya ziada kwa waajiriwa na waajiri ili kuongeza ufanisi katika kazi”.

0 Responses to “ONGEZEKO LA BAJETI KATIKA SEKTA YA UTALII”

Post a Comment

More to Read