Sunday, January 31, 2016

ATAKAYEKATA MTI KUKIONA CHA MOTO.MBEYA


Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mh Nyirembe Munasa akiwa ameshika Miti na kupanda Mlima kwaajili ya kupanda(Picha na David Nyembe wa Fahari News)


Maafisa Habari wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Bi Jaqueline Msuya na John kilua na hawakuwa Nyuma katika zoezi la kupanda Miti


Kuelekea kwenye Chanzo Chanzo cha Maji Mto Simba(Picha na David Nyembe wa Fahari News)

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mjini Mh Nyirembe Munasa(aliyeshika Jembe)akitoa maelekezo kwa Madiwani(Picha na David Nyembe wa Fahari News)

wakishuka mitelemko na mabonde kupamba Miti katika chanzo cha Mto Simba kilichop[o Kata ya Mwakibete jijini Mbeya(Picha na David Nyembe wa Fahari News)

Nao walikuwepo kutekeleza agizo la Serikali kupanda Miti

Afisa Habari  wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Bi Jaqueline Msuya akipanda Mti.


Diwani wa Kata ya Forest Mh Henry Mwangambako  akitoa Shukrani kwa Wananchi kwa Niaba ya Meya wa Jiji la Mbeya  walioshiriki zoezi la Kupanda Miti katika Chanzo cha Maji cha  Mto Simba kilichopo katika kata ya Mwakibete(Picha na David Nyembe wa Fahari News)


Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Akitoa Neno la Shukrani (Picha na David Nyembe wa Fahari News)





SERIKALI wilayani Mbeya imeonya kuwa haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wananchi watakaoharibu kwa makusudi miti iliyopandwa ndani ya mita 60 kutoka kilipo chanzo cha maji.

Onyo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki  na mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyerembe Munasa  wakati wa uzinduzi wa siku ya upandaji miti iliyofanyika kwenye chanzo cha mto Simba, kata ya Mwakibete jijini hapa.

Alisema kuwa kukata miti kwenye vyanzo vya maji kunakwamisha jitihada za serikali za uhifadhi wa mazingira na kwamba atakayebainika kufanya vitendo hivyo  serikali  haitasita kumfikisha mahakamani au kumtoza faini.

“Nimeelezwa kuwa kuna tabia ya baadhi ya wananchi wanang’oa, kufukia, kuchungia au kuharibu kwa namna yoyote miti iliyopandwa kiasi kwamba kampeni hizi zinakuwa hazina maana watakaofanya vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kulipa faini au kufikishwa mahakamani” alisema.

Alisema kuwa sheria ya misitu namba 14 ya mwaka 2002 na sheria ya ya usimamizi wa mazingira namba 20 ya mwaka 2004 zinatoa maelekezo juu ya usimamizi na utunzaji wa vyanzo vya maji na misitu. “napenda kusisitiza ni marufuku ndani ya mita 60 kufanya shughuli yoyote ya kibinadamu inayoweza kuhatarisha au kuathiri chanzo chohote cha maji” alisisitiza.

Mkuu huyo wa wilaya alimtaka kila mmiliki wa eneo kupanda miti isiyopungua mitano katika eneo lake na kuitunza mpaka ikue kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho.

Awali kaimu mkurugenzi wa jiji la Mbeya Dr. Samwel Lazaro aliiomba serikali kuhakikisha kuwa masuala ya misitu yanapewa nafasi muhimu katika upangaji na utekelezaji wa sera za maendeleo.

Alisema ni vyema serikali za mitaa zikaimarishwa ili kusimamia rasilimali za misitu na kunakuwapo na mbinu za utaratibu baina ya serikali kuu na serikali za mitaa.

Dr. Lazaro alisema kuwa katika uzinduzi huo jumla ya miti 4000 imepandwa katika eneo hilo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali kuhusu uhifadhi wa misitu na vyanzo vya maji.

MWISHO

0 Responses to “ATAKAYEKATA MTI KUKIONA CHA MOTO.MBEYA”

Post a Comment

More to Read