Monday, June 16, 2014
SIKU YA MTOTO WA AFRIKA WILAYANI MAKETE, MKUU WA WILAYA AIOMBA JAMII KUWASAIDIA WATOTO YATIMA NA WAISHIO KWENYE MAZINGIRA HATARISHI
Do you like this story?
Imeelezwa
kuwa ni jukumu la kila mmoja kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika
mazingira hatarishi, na si kuiachia serikali ama mashirika yasiyo ya kiserikali
peke yao kufanya kazi hiyo
Kauli
hiyo imetolewa leo hii Juni 16 na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro
ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika
yaliyofanyika kitaifa (kwa asasi zisizo za kiserikali) katika viwanja vya
mabehewani kata ya Iwawa wilayani Makete mkoani Njombe
Hata
hivyo mkuu wa wilaya hiyo amekiri kuwepo kwa changamoto ya watoto walio wengi
Wilayani Makete ambao ni Yatima na waishio katika mazingira magumu ambao
wanahitaji msaada wa kila mmoja
"Ni
kweli wilaya ya Makete ina watoto ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira
hatarishi, wengine wanalelewa katika vituo maalum vilivyopo wilayani mwetu,
hivyo ni jukumu letu kuwasaidia kila mtu kwa kadri ya uwezo wake, mwenye
sabuni, kalamu, fedha ama chochote anaweza kufanya hivyo kwa wakati wake"
amesema Matiro
Katika risala iliyosomwa na mwanafunzi Gaudencia Malangalila wa Shule ya msingi Ndulamo kwa niaba ya wanafunzi wenzake amesema Kuwa watoto walio wengi wanakabiliwa na unyanyasaji kwa kufanyishwa Kazi ngumu na hatarishi,kutopata haki katika huduma za matibabu,walezi kunyang'anya misaada wanayopewa na wadau mbalimbali
Naye Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) Bi. Helen Kijo Bisimba amesema Kuwa kwa Tafiti alizofanya amebaini Kuwa kuna watoto ambao waliondoka kwenda nje ya Makete kwa kufanya Kazi na hawarudi tena huku wazazi hawajui Kama wapo hai au la,kwani hata mawasiliano na wazazi ama walezi wao bado ni magumu
Hivyo amewasihi wazazi/walezi Kuwa makini na watoto wao pindi wanapoitwa kwenda kufanya Kazi maeneo ya mbali kwani mara nyingi huko wanakokwenda wanakutana na mambo ambayo ni kinyume na walioyatarajia
Katika maadhimisho hayo kikundi cha wazazi kutoka Kijiji cha Isapulano na Ndulamo Maarufu Kama mama mkubwa wamesema Kuwa vikundi hivyo vitaendelea Kulinda haki za watoto na kutoa ujumbe kwa jamii kwa njia ya sanaa na kufanya uchunguzi dhidi ya watoto wanaofanyiwa unyanyasaji na watatoa taarifa katika ngazi husika na wakigundulikaa wahusika wachukuliwe hatua za kisheria
Kauli
mbiu ya mwaka huu ni "kila mtoto ana haki ya elimu bora bila vikwazo"
Chanzo>Eddy Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SIKU YA MTOTO WA AFRIKA WILAYANI MAKETE, MKUU WA WILAYA AIOMBA JAMII KUWASAIDIA WATOTO YATIMA NA WAISHIO KWENYE MAZINGIRA HATARISHI ”
Post a Comment